Katibu
wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani Nd. Epi Fania Ngonyani
akibadilishana mawazo na Balozi Seif akijiandaa na ujumbe wake kuondoka
Bandarini Malindi kurejea Mjini Dar es salaam baada ya kumaliza ziara
yao ya ujirani mwema. Nyuma ya Ndugu Ngonyaji ni Mwenyekiti wa CCM wa
Tawi hilo Ndugu Haroub Othman Mberwa.
Balozi
Seif akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makangira Ndugu Haroub
Othman Mberwa aliyeuongoza ujumbe wa Viongozi kumi wa Kata hiyo
waliofanya ziara ya ujirani mwema hapa Zanzibar.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhKZCv_QfWCOsT-4HAVOJAm2rL4zOuWTCREnJCjpzNUwt_Rb8ohUHRToqlaj0z0FqN_dzklaRpOF1J8KRjwmcR21KktBxGJWQRm-dLKwszUW2SmjsUjb46qmoQ2vsvLowg0LeCYZjgWxjQ/s640/352.jpg)
Viongozi
na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Matawi mbali mbali Nchini
Tanzania wanapaswa kuwa makini katika kuwachangua viongozi imara wakati
utakapowadia wa chaguzi za Chama hicho ili kuirahisisha kazi ya ushindi
CCM mwaka 2020.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani
Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Haroub Othman Mberwa
wakati akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi hapo Bandarini Malindi
Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti
Mberwa na Ujumbe wake wa Viongozi Kumi wa Kata ya Makangira Msasani
ulikuwepo Zanzibar kwa ziara ya kuimarisha uhusiano mwema kati ya kata
hiyo na wenyeji wao wa Tawi la CCM Vikokotoni lilioko Mji Mkongwe
Zanzibar.
Ndugu
Mberwa alisema wakati umefika kwa wana CCM kuendelea kuongozwa na
Viongozi makini waliobobea hekima na busara kuanzia Matawi maeneo ambayo
ni chimbuko halisi la upatikanaji wa Viongozi katika ngazi za Majimbo,
Wilaya, Mkoa hadi Taifa.
Alisema
Chama cha Mapinduzi kimepata misukosuko mingi katika awamu tofauti za
Uongozi zilizopita iliyosababishwa na baadhi ya Viongozi wenye sura
mbili za maamuzi jambo ambalo lilipelekea kuwa na mgawanyiko na hatimae
kuzalisha makundi yaliyozaa ufa ndani ya chama hicho.
Ndugu
Mberwa alitahadharisha kwamba Wanachama wa CCM Matawini ndio wenye kauli
na rungu za kuwachagua Viongozi watakaokuwa tayari kuwatumikia katika
misingi ya uadilifu na ni vyema kuachana na tabia ya kubebana kwa
kisingizio cha ukabila, uzawa na urafiki.
Alieleza
kwamba tabia kama hizo ndizo zinazopelekea Viongozi wa Kitaifa
kukumbana na wakati mgumu katika kutoa maamuzi ya hatma ya muelekeo wa
kumpata Kiongozi wa kubeba dhamana ya kuwatumikia katika masuala yao ya
Chama.
Naye
Katibu wa Tawi la CCM la Makangira Kata ya Msasani, Wilaya ya Kiondoni
Mkoa wa Dar es salaam Nd. Epi Fania Ngonyani alisema uwepo wa ujumbe wao
hapa Zanzibar umejifunza mambo mengi yatakayosaidia kuimarisha chama
chao kwa upande wa Tanzania Bara.
Nd.
Ngonyani alisema matembezi ya sehemu za kihistoria pamoja na Mikutano ya
hadhara ya kukutana na wanachama wenzao wa baadhi ya Matawi na hata
Wilaya za Tanzania Zanzibar imewajengea heshima na upendo kati yao na
wenyeji wao iliyopelekea pia kujadili mapungufu yaliyojitokeza wakati wa
uchaguzi mkuu uliopita.
Alieleza
kwamba katika mikutano hiyo ya uhusiano mwema pande hizo mbili
zilipendekeza uwepo wa mikakati ya makusudi ya kujengewa uwezo zaidi wa
uwezeshaji makundi makubwa ya vijana na wanawake ili washiriki vyema
kwenye shughuli za uzalishaji.
Ziara
hizo za kuimarisha uhusiano mwema kati ya Matawi ya Chama cha Mapinduzi
ya Vikokotoni Mjini Zanzibar na Makangira Msasani Dar es salaam
hufanyika kwa kutembeleana kila mwaka.
No comments:
Post a Comment