Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe wakitoka kukagua nyumba za TBC ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani.
: Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe
Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika
kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za
watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa
maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge
Hostel za wanafunzi.
Moja ya nyumba za TBC ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani. Kaimu Mkurugenzi Mkuu /Mkurugenzi rasilimali Watu na Uendeshaji wa TBC Bi.Joycelin Lugora akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani), kulia ni Mkurugenzi wa wilaya ya Kisarawe (DED) Kisarawe Bi. Mwanamvua Mlindoko na kushoto ni Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBC na Wanahabari wakitoka kujionea hali halisi wakati Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mhe. Anastazia Wambura pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kisarawe alipokwenda kukagua nyumba za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), ambazo ujenzi wake umekwama kwa zaidi ya miaka 21 zilizopo Kisarawe mkoani Pwani.PICHA NA ANNA NKINDA.
Wambura-Sitakubali Rasilimali za Taifa hili zichezewe.
Na.Daudi Manongi-WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)
kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi
na ingeweza kutumika kwa kazi nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika
kiwanja cha Shirika hilo kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za
wafanyakazi wa shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.
Mhe.Wambura
alisema hayo wakati alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa
maagizo aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011
mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo ikishirikiana
na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo hilo
la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
“Taratibu
za Kisarawe za upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu
kwa kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba kulikuwa
na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa lakini kwa sasa hivi
bado tunaitaji kulinda rasilimali za Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu”,Alisema
Mhe Wambura.
Aidha
Mhe Wambura ametoa maagizo kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza
makazi hayo kwa kuwa mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na
shirika hilo au kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa
halmashauri ya kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye
hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi kubomoa nondo na kuuza kama vyuma chakavu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji
Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha
kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa na kudai kwamba mara nyingi wanaweka pesa ya
ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya
Arusha na Mwanza na makao makuu kwa hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa
mara moja.
No comments:
Post a Comment