Jaji
Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa
Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake
kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma..
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika
Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara
baada ya tukio la uapisho. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment