HAWA NI AKINA MAMA WA MTAA WA KIBENA HOSPITALI WAKISHEREKEA KUPATA KISIMA CHA MAJI
HAPA SASA WANAFURAHIA HUDUMA YA MAJI YA KISIMA KILICHOCHIMBWA NA KAMPUNI YA TANWAT NJOMBE
KULIA NI AFISA UTAWALA WA TANWAT EDMUND MNUBI,WA PILI KUTOKA KULIA NI KAIMU MKURUGENZI WA KAMPUNI YA TANWAT DKT RAJEEV SINGH NA WA TATU KUTOKA KULIA NI MENEJA MKUU WA MISITU KATIKA KAMPUNI HIYO ANTERY KIWALE.
AFISA MTENDAJI WA MTAA WA KIBENA HOSPITALI COLUMBA MSEMWA AKISOMA TAARIFA FUPI KWA MGENI RASMI
KULIA NI MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA KIBENA HOSPITALI WINFRED KAYOMBO,NA WA PILI KUTOKA KULIA NI DIWANI KATA YA RAMADHANI GEOGE MENSON SANGA
HIKI NDIYO KISIMA AMBACHO KIMEKABIDHIWA KWA WANANCHI WA KIBENA HOSPITALI NA KAMPUNI YA TANWAT NJOMBE
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA KIBENA HOSPITALI AKIWA NA DIWANI WA KATA HIYO WAKIFURAHI NA KUPEANA MIKONO KWA KUFANIKISHA KUPATA KISIMA HICHO
KAIM MKURUGENZI WA TANWAT DKT RAJEEV SINGH AKIWA NA AFISA UTAWALA WA KAMPUNI HIYO AKITOA HOTUBA YAKE
Mkurugenzi Wa Kampuni Ya Tanwat Mjini Njombe Dkt Rajeev Singh Ameahidi Kutoa Msaada Wa Mbao
Zaidi Ya Mia Nne Kwaajili Ya Kukamilishia Jengo La Ofisi Ya Serikali Ya Mtaa Wa Kibena Hospitali
Ambapo Amesema Kampuni Hiyo Inatoa Misaada Endapo Wananchi Wataonesha Mfano Wa Kuanza
Utekelezaji Wa Miradi Iliyopewa Kipaumbele.
Kaimu Mkurugenzi Wa Kampuni Ya Tanwat Dkt Rajeev Singh Akitafsiliwa Lugha Na Afisa Utawala Wa
Kampuni Hiyo Edmund Munubi Amepongeza Serikali Ya Mtaa Wa Kibena Hospitali Kwa Jitihada
Walizofanya Za Kuomba Kusaidiwa Kuchimbiwa Kisima Hicho Ambapo Kutokana Na Juhudi Za Wananchi
Walizoonesha Ameahidi KutoaMbao Zaidi Ya Mia Nne Kwaajili Ya Ofisi Ya Serikali Ya Mtaa Huo.
Dkt Singh Pia Amekabidhi Mradi Wa Maji Ya Kisima Kwa Uongozi Wa Mtaa Wa Kibena Hospitali
Uliogharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni Mbili Ambapo Kukabidhiwa Kwa Mradi Huo Kutasaidia Kutatua
Changamoto Ya Ukosefu Wa Maji Iliyokuwa Ikiwakabili Wakazi Wa Eneo Hilo Kwa Kipindi Cha Muda
Mrefu.
Kwa Upande Wake Meneja Mkuu Wa Misitu Wa Kampuni Ya Tanwat Antery Kiwale Akizungumza Wakati
Wa Kukabidhi Mradi Huo Amewataka Wananchi Kuonesha Ushirikiano Katika Kuilinda Misitu Ya
Kampuni Hiyo Kwa Kukemea Tabia Ya Uchomaji Hovyo Wa Moto Pamoja Na Kuwataja Baadhi Ya Watu
Wanaojihusisha Na Wizi Wa Magogo Ya Mbao .
Diwani Wa Kata Ya Ramadhani Geoge Menson Sanga Ameshukuru Wananchi Kwa Kujitokeza Kwa Wingi
Katika Kushiriki Ujenzi Wa Ofisi Ya Mtaa Huo Ambapo Pia Amepongeza Kampuni Ya Tanwat Kwa
Kuwakabidhi Kisima Hicho Pamoja Na Ahadi Ya Kuwapatia Zaidi Ya Mbao Mia Nne Kwaajili Ya Jengo La
Ofisi Hiyo.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Serikali Ya Mtaa Wa Kibena Hospitali Winfred Kayombo Pamoja Na
Kushukuru Kwa Kukabidhiwa Mradi Huo Lakini Amesema Serikali Itasimamia Matumizi Sahihi Ya Kisima
Hicho Ili Wananchi Wanufaike Wote Kwa Kuwa Na Matumizi Mazuri Na Kisima Hicho Kidumu Kwa Muda
Mrefu.
Awali Akisoma Risala Fupi Mbele Ya Mgeni Rasmi Afisa Mtendaji Wa Mtaa Wa Kibena Hospitali Bi.
Columba Msemwa Amesema Katika Kutekeleza Mradi Wa Maji Ya Kisima Hicho Wananchi Wamechangia
Kiasi Cha Zaidi Ya Shilingi Laki Mbili Huku Ujenzi Wa Jengo La Ofisi Wakichangia Zaidi Ya Shilingi milini
Sita Na Fedha Nyingine Imepatikana Mfuko Wa Maendeleo Ya Kata Ambapo Hadi Lilipofikia Hatua Ya
Bimu Limegharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni Tisa.
Wananchi Wa Mtaa Wa Kibena Washukuru Kwa Kukabidhiwa Kisima Hicho Ambacho Kimetajwa Kutatua
Changamoto Ya Kukosekana Kwa Huduma Za Maji Katika Mtaa Huo Na Kuahidi Kuonesha Ushirikiano
Mkubwa Kwa Kampuni Hiyo Kwani Imeonesha Upendo Wa Kutosha Kwao.
No comments:
Post a Comment