Wednesday, May 11, 2016
KIJANA MMOJA MKAZI WA IGAGALA WILAYA YA WANGING'OMBE AKUTWA AMEFARIKI LEO KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KYENYEJI NJOMBE MJINI
MWILI WA KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 32 FIDELISI MHEPELA ULIPOKUTWA ASUBUHI YA LEO KWENYE KILABU CHA POMBE ZA KYENYEJI CHA NDEVALONGE AMBAKO ALIKUWA ANALALA BAADA YA KUKOSA MAKAZI MJINI NJOMBE.
BAADHI YA WANANCHI WAKIPANDA KWENYE GARI LA POLISI ILI KWENDA KUSAIDIA KUTOA MWILI HUO KUWEKA KWENYE CHUMBA CHA MAITI KIBENA ILI NDUGU ZAKE WAFIKE KUUCHUKUA KWAAJILI YA MAZISHI
MASHUHUDA WAKIPANDA KWENYE GARI LA POLISI ASUBUHI YA LEO
HUU NI MLANGO WA CHUMBA CHA BIASHARA ALICHOKUWA AKILALA BAADA YA WATEJA KUONDOKA ALIMOKUTWA MAREHEMU AKIWA AMEFARIKI DUNIA
Mkazi Mmoja Wa Kijiji Cha Igagala Kata Ya Ulembwe Wilayani Wanging'ombe Fiderisi Mhepela Mwenye Umri Wa Miaka 32 Amekutwa Akiwa Amefariki Dunia Kwenye Kilabu Cha Pombe Za Kyenyeji Cha Ndevalonge Kilichopo Mtaa Wa Mpechi Eneo La Lutilage Mjini Njombe Ambapo Mwili Wake Upelekwa Kuhifadhiwa Katika Chumba Cha Maiti Cha Hospitali Ya Mkoa Wa Njombe Ya Kibena.
Wakizungumza Mapema Leo Baadhi Ya Wananchi Na Mashuhuda Wa Tukio Hilo Wamesema Mwili Wa Marehemu Fidelis Mhepela Umekutwa Asubuhi Ya Leo Ukiwa Chini Ya Sakafu Ya Chumba Cha Biashara Ya Pombe Za Kyenyeji Ambacho Alikuwa Akilala Kama Mlinzi Baada Ya Kuomba Kwa Wamiliki Kwamba Hana Sehemu Ya Kuishi Huku Milango Yote Akiwa Amefunga .
Aidha Mashuhuda Hao Wamesema Mara Nyingi Marehemu Alikuwa Akilala Kwenye Chumba Hicho Na Asubuhi Anaendelea Na Shughuli Za Kufanya Vibarua Vya Kusomba Pombe Na Kwenda Kulima Kwa Watu Tofauti Tofauti Na Kisha Jioni Anarudi Kujihifadhi Kwenye Kilabu Hicho Ambacho Mauti Yake Ymemkuta Usiku Wa Kuamkia Leo Pasipo Wafanyabiashara W a Eneo Hilo Kufahamu Chanzo Cha Kifo Chake .
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Wa Mpechi Deogratias Msemwa Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Katika Mtaa Wake Na Kusema Kuwa Chanzo Cha Kifo Hicho Hakijafahamika Ambapo Jukumu La Kufanya Uchunguzi Wa Tukio Hilo Wameliachia Jeshi La Polisi Litakalo Toa Taafira Ya Kifo Hicho Baada Ya Kupata Taarifa Ya Daktari.
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Limefika Kwenye Tukio Hapo Kwa Wakati Ili Kuimarisha Ulinzi Na Usalaama Na Kuchakua Mwili Wa Kijana Huyo Kwaajili Ya Kuhifadhi Kwenye Chumba Cha Maiti Kibena Huku Uchunguzi Wa Tukio Hilo Ukiendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment