WATU
WANNE WANAOZANIWA KUWA NI WEZI WALIVAMIA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA WA
MBAO SILVIA OSCAR NA KUJERUHI WATU WAWILI HUKO IGOMBE WILAYANI ILEMELA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA.
MWANAMKE
MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JULIANA MASHIKO MIAKA 41 MKULIMA NA
MKAZI WA KIJIJI CHA KIZUGWANGOMA ALIJERUHIWA KWA KUKATWA NA PANGA KWENYE
BEGA LA MKONO WA KULIA NA MATHIAS SALIANA MIAKA 19 HALI ILIYOPELEKEA
KURUPUSHANI NA YOWE AKIOMBA MSAADA KUTOKA KWA MAJIRANI ILI WAWEZE
KUMSAIDIA. TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.05.2016 MAJIRA YA
02:30HRS KATIKA KIJIJI NA KATA YA KIZUGWANGOMA WILAYA YA SENGEREMA MKOA
WA MWANZA.
INADAIWA
KUWA MATHIAS SALIANA ALIKWENDA NYUMBANI KWA BI JULIANA AKIWA NA PANGA
AKIDAI APEWE FEDHA KWA LAZIMA HUKU MWANAMKE HUYO AKIGOMA NAKUAMUA
KUMKATA PANGA BI JULIANA KWENYE BEGA LA MKONO WA KULIA NDIPO MWANAMKE
HUYO ALIANZA KUPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA KUTOKA KWA MAJIRANI, NDIPO
MAJIRANI WALIFIKA NA KUMSAIDIA MAMA HUYO.
AIDHA
BAADA YA KUMSAIDIA BI JULIANA, WANANCHI HAO WALIMKAMATA KIJANA HUYO NA
KUMPIGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA WAKAMFIKISHA KWENYE KITUO
CHA POLISI AKIWA NA HALI MBAYA KIAFYA NA KUPELEKEA KWENDA KULAZWA
HOSPITALI YA MISHENI YA WILAYA YA SENGEREMA AKIWA CHINI YA ULINZI WA
ASKARI POLISI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KILA MMOJA KUWA MLINZI WA MWENZAKE
KATIKA KUPAMBANA NA UHALIFU KATIKA MKOA WETU WA MWANZA. LAKINI PIA
AKIWATAKA WANANCHI KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BALI WATOE
USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI PINDI WANAPOMKAMATA MHALIFU ILI AWEZE
KUFIKISHWA POLISI NA KUCHUKULIWA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ILI IWE MFANO
KWA WATU WENGINE.
KATIKA TUKIO LA PILI.
WATU
WANNE WANAOZANIWA KUWA NI WEZI WALIVAMIA NYUMBANI KWA MFANYA BIASHARA WA
MBAO WA KIGOTE – IGOMBE ANAYEJULIKANA KWA JINA LA BI SILVIA OSCAR MIAKA
30 NA KUMJERUHI KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI KWENYE KIGANJA CHA
MKONO WA KUSHOTO, AKAFANIKIWA KUJIOKOA KWA KUKIMBIA NA KUWAACHA WATU
HAO NDANI YA NYUMBA. NDIPO WALIPOKUTANA NA BABA MZAZI WA SILVIA
ANAEISHINAE HAPO NYUMBANI KWAKE AITWAYE OSCAR MKAIMA MIAKA 57 AMBAYE
WALIMJERUHI KIDOGO KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI. TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 12.05.2016 MAJIRA YA SAA 20:40HRS USIKU
KATIKA MTAA WA KITOGE- IGOMBE KATA YA BUGOGWA WILAYANI ILEMELA MKOANI
MWANZA.
INADAIWA
KUWA WAHALIFU HAO WALIINGIA NDANI YA NYUMBA HIYO NA KUWAKUTA WENYE KAYA
WAKIWA WANAKULA CHAKULA, HAWAKUCHUKUA KITU CHOCHOTE. MAJERUHI
WAMETIBIWA NA KURUHUSIWA KURUDI NYUMBANI, WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO DHIDI YA TUKIO HILO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
MSANGI AMESEMA “JESHI LA POLISI LINAFANYA MSAKO MKALI WA KUWATAFUTA WATU
WALIOHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KWENYE TUKIO HILO NA KUHAKIKISHA
WANAKAMATWA,” PIA AMETOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU AU
UHALIFU MAPEMA ILI WAHALIFU WAWEZWE KUKAMATWA NA KUSHUGHULIKIWA KWA
MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI ZINAVYO ELEKEZA.
Imesainiwa na. SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
No comments:
Post a Comment