MWENYEKITI WA CHAMA CHA USHIRIKA MKOA WA NJOMBE NJORECU CLEMENCE MALEKELA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI AWEZE KUZUNGUMZA NA WAKULIMA HAO
MWEZESHAJI WA SEMINA KUTOKA SSRA MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM BI. SARAH KIBONDE MJULA
MRAJISI WA VYAMA VYA USHIRIKA MKOA WA NJOMBE EXAUD SAPALI NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA USHIRIKA MKOA WA NJOMBE CLEMENCE MALEKELA WAKITETA JAMBO KABLA YA KUANZA KWA SEMINA
MRAJISI AKIWA MGENI RASMI KWENYE SEMINA YA LEO
PICHA YA PAMOJA NA WAKULIMA WALIOHUDHURIA SEMINA HIYO LEO NJOMBE
Mamlaka Ya Usimamizi Na Udhibiti Wa Sekta Ya Hifadhi Ya Jamii Imewataka Wakulima,Wafanyabiashara Na Wananchi Kujiunga Na Mifuko Ya Taifa Ya Hifadhi Ya Jamii Iliyopo Hapa Nchini Ili Waweze Kunufaika Na Mafao Ya Uzeeni Pamoja Na Kupatiwa Mikopo Ya Kuendeshea Shughuli Zao Za Kiuchumi Kwa Wanaohitaji Mikopo.
Akizungumza Wakati Wakufanga Semina Ya Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii Kwa Shirikisho La Wakulima Mkoa Wa Njombe, Mrajisi Wa Vyama Vya Ushirika Exaud Sapali Ametaka Wananchi Kujiunga Na Mifuko Ya Hifadhi Ya Jamii Kwaajili Ya Kunufaika Na Matibu Bure Katika Hospitali Na Vituo Vya Afya Pamoja Na Kupata Mafao Ya Uzeeni Watakayopata Wakistaafu Kazi.
Aidha Bwana Sapali Pia Ametaka Wakulima Hao Kujiunga Na Vyama Vya Ushirika Vilivyopo Kwenye Maeneo Yao Ambavyo Vitakuwa Vinawasaidia Kuwakopesha Mikopo Yenye Riba Nafuu Kwaajili Ya Kuinua Uchumi Wa Kila Mmoja Huku Akisema Serikali Imekwisha Fufua Chama Cha Ushirika Cha Mkoa Wa Njombe NJORECU Kinachounganisha Halmashauri Zote Ambacho Kilitelekezwa Tangu Mwaka 1994.
Akitoa Semina Ya Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii Kwa Shirikisho La Wakulima Mkoa Wa Njombe Mkurugenzi Wa Mawasiliano Na Uhamasishaji Wa Mamlaka Ya SSRA Bi. Sarah Kibonde Mjula Amesema Kuna Mifuko Saba Ya Hifadhi Ya Jamii Ambayo Ilianzishwa Na Serikali Kwa Lengo La Kukabiliana Na Majanga Mbalimbali Yatakayojitokeza Huku Akizitaja Nguzo Kuu Tatu Na Kuzifafanua Zaidi .
Wakizungumza Na Uplands Fm Mara Baada Ya Semina Hiyo Baadhi Ya Wakulima Wameshukuru Kwa Kupatiwa Elimu Ya Kujiunga Na Mifuko Mbalimbali Ya Hifadhi Ya Jamii Na Kuahidi Kujiunga Kwani Wametambua Umuhimu Wa Mifuko Hiyo Huku Wengine Wakiwa Na Hofu Kwa Kufikisha Matatizo Yao Yakitokea Baina Ya Mifuko Hiyo Kutokana Na Ofisi Za SSRA Kuwa Dar Es Salaamu Kama Ofisi Nyingine.
Clemence Malekela Ni Mwenyekiti Wa Chama Cha Ushirika Mkoa Wa Njombe NJORECU Amewashukuru Wakulima Hao Walioshiriki Semina Hiyo Kwani Wamepata Elimu Ya Kutosha Juu Ya Umuhimu Wa Vyama Vya Ushirika Na Kujiunga Na Mifuko Ya Taifa Ya Hifadhi Ya Jamii Na Kutaka Kuwashawishi Wakulima Wengine Kujiunga Na Vyama Vya Ushirika Vilivyopo Karibu Nao Ili Waunganishwe Na Mifuko Ya Hifadhi Ya Taifa Ya Jamii .
No comments:
Post a Comment