Mtaalam
wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja
akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa
Tanzania.kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo.
Mkurugenzi
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw.
Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa
bei nchini kwa mwezi Aprili 2016 leo jijini Dar es salaam, Kulia ni
Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji
Semboja.Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 umepungua hadi
asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.4.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu, ya Jamii).
Na. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
OFISI
ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili
2016 na kusema kuwa umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka
asilimia 5.4 iliyokuwepo mwezi Machi, 2016.
Hii
inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi
Aprili 2016 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei
ya bidhaa na huduma iliyokuwepo mwezi Machi mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Bw. Ephraim Kwesigabo ametoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam na
kueleza kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa
kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika
maeneo mbalimbali nchini.
Amesema
Takwimu zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwenye bidhaa
zinazotumika kupima mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2016 zimeainisha
kuwa bidhaa zisizo za vyakula katika soko zikiwemo Gesi , dizeli na
mafuta ya taa zimechangia kupungua kwa mfumuko huo.
Amesema
kuwa pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa hizo kwa
mwezi Aprili 2016, baadhi ya bidhaa za vyakula ikiwemo mchele, unga wa
Mahindi na mkaa ilionyesha kuongezeka katika kipindi hicho.
Akizungumzia
Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima
mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa
Tanzania kwa mwezi Machi na Aprili Bw. Kwesigabo amesema kuwa
zimeongezeka hadi kufikia 102.46 kutoka 101:93 za mwezi Aprili.
Amesema
kuwa tofauti na mwezi Machi bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka
kwa fahirisi kwa mwezi Aprili ni unga wa muhogo, dagaa, choroko, maziwa
ya ungana na matunda aina ya machungwa.
Aidha,bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mvinyo, bia kuni na mazulia.
Kwa
upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na
huduma za mlaji kwa mwezi Aprili, 2016 umefikia shilingi 97 na senti 60
ikilinganishwa na uwezo wa shilingi 98 na senti 11 wa mwezi Machi 2016.
“Uwezo
wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile
kwa mlaji kwa mwezi Aprili 2016 umepungua, hii ina maana kuwa sasa mtu
anahitaji kuongeza ya shilingi 2.40 ili aweze kununua bidhaa na huduma
sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Machi " Amesema
Kwesigabo.
Kwa
upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki mwezi Machi, 2016,
Kwesigabo amesema una mwelekeo unaofanana; Kenya umepungua kidogo hadi
kufikia asilimia 5.27 kutoka 6.45 huku Uganda ukifikia asilimia 5.1
kutoka asilimia 6.2 zIlizokuwepo mwezi Machi 2016.
No comments:
Post a Comment