Kauli Hiyo Imetolewa Na Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Pudensiana Plotas Wakati Akizungumza Na Uplands Fm Kuhusiana Na Namna Jeshi Hilo Lilivyo Jipanga Kuhakikisha Matukio Ya Uharifu Hayaendelei Kwa Kasi Ambapo Amesema Doria Zimeendelea Kufanyika Kila Mahala Na Kutaka Wananchi Kushirikiana Kwa Pamoja Kutokomeza Vitendo Hivyo.
Aidha Kamanda Plotas Amesema Jeshi La Polisi Bado Linaendelea Na Msako Wa Kuwabaini Waharifu Waliosababisha Matukio Mawili Ya Mauaji Katika Mtaa Wa Idundilanga Na Ngaranga Kwenye Shule Ya Sekondari Wende Na Kuzuia Waharifu Wengine Ambao Wanatarajia Kufanya Matukio Na Kuimarisha Taarifa Za Kiiteligensia Kubaini Wahusika Waliko.
Hata Hivyo Ameshauri Wakulima Na Wafanyabiashara Wa Mkoa Wa Njombe Kuzitumia Zaidi Taasisi Za Kifedha Kuhifadhi Pesa Zao Pindi Wanapouza Mazao Yao Huku Akisema Wafanyabiashara Wanatakiwa Kuzingatia Muda Wa Kuuza Biashara Zao Kwa Kutouza Hadi Usiku Wa Manane Ili Kuwaepusha Na Matukio Yanayoweza Kujitokeza Ya Uvunjifu Wa Amani.
Baadhi Ya Wananchi Mjini Njombe Wameomba Jeshi La Polisi Kufanya Doria Shemu Mbalimbali Zikiwemo Za Vyombo Vya Usafiri Kukagua Silaha Na Watu Wanaokwenda Kufanya Uharifu Sehemu Frani Kwani Matukio Ya Mauaji Yanayofanywa Na Majambazi Yanatokana Na Jeshi La Polisi Kushindwa Kukagua Mizigo Ya Abiria Wanaosafiri Kwenye Mabasi Na Magari .
No comments:
Post a Comment