MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKIZUNGUMZA HII LEO OFISINI KWAKE JUU YA KIFO CHA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE MAREHEMU SARAH DUMBA
BAADA YA KUPATWA NA HALI YA KUKOSA HEWA NA KUTAPIKA MAREHEMU ALIPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA KIBENA NJOMBE KWA MATIBABU NA NDIPO ALIPOGUNDULIKA AKIWA AMEFARIKI DUNIA
MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG TANZANIA ASSEMBLES OF GOD CEFANIA TWEVE AKIWA NYUMBANI KWA MAREHEMU AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI
EDWIN KILASI ALIKUWA KATIBU WA UHAMASISHAJI WA MAJI NYENGA AMEMUELEZEA MAREHEMU SARAH DUMBA KWAMBA NI MIONGONGI MWA VIONGOZI WALIOSHIRIKI KUHAMASISHA UCHANGIAJI WA MRADI WA MAJI NYENGA YASOGEZWE NJOMBE MJINI KWA KUCHANGIA ELFU 30 KILA MMOJA MWENYE MAPENZI MEMA.
.......................................................................................................................................................................
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi Ameelezea Kifo cha Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Marehemu Sara Dumba Aliyefariki Jana Usiku Katika Hospitali ya Mkoa Huo (Kibeana) Wakati Akipatiwa Matibabu Baada ya Kuugua Ghafla.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake Dkt. Nchimbi Amesema Mwili wa Marehemu Utasafirishwa Kwenda Jijini Dar Es Salaam Kwa Ajili ya Mazishi, na Kwamba Kabala ya Kusafirishwa Mwili wa Marehemu Sara Dumba Utapelekwa Katika Kanisa la KKKT Mjini Njombe Kwa Ajili ya Misa ya Mazishi.
Nao Baadhi ya Wananchi , Viongozi wa Dini, Serikali na Siasa Waliozungumza na Upland's Redio Wameelezea Namna Walivyokuwa Wakishirikiana na Marehemu Wakati wa Uhai Wake Katika Kutekeleza Miradi ya Maendeleo Pasipo Kujali Itikadi Zao.
Kabla ya Kuteuliwa Kushika Wadhifa wa Ukuu wa Wilaya Marehemu Sara Dumba Alikuwa Mtangazaji wa Shirika la Habari Tanzania Kipindi Kili Ilijulikana Kama Redio Tanzania Dar Es Salaam (RTD).
Mungu Alitoa na Mungu Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe, Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Ma Hali Pema Peponi , Amen
No comments:
Post a Comment