Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) lina sikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali January
Claudio Kisanko (mstaafu) kilichotokea tarehe 21Machi 2016,
Meja Jenerali January Kisanko
(mstaafu) alizaliwa mwaka 1945 katika kijiji cha Mkima, Tarafa ya
Lyangalile, Wilaya ya Sumbawanga. Alipata Elimu ya Msingi Mkoani Rukwa
na baadaye elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya wavulana
Agakhan ambayo kwa sasa ni shule ya Sekondari Tambaza, hadi alipohitimu
kidato cha Sita mwaka 1966.
Marehemu Meja Jenerali January
Claudio Kisanko (Mstaafu) alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania tarehe 31 Mei, 1967 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 24 Julai,
1969.Marehemu alilitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 35 na mwezi 1 hadi
alipostaafu utumishi Jeshini tarehe 30 Juni 2002.
Katika utumishi wake marehemu
alishika Madaraka mbalimbali Ikiwemo Kamanda wa patuni Nachingwea 1969
hadi 1970, Kamishina wa Mipango na Sera katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa 2001, madaraka ambayo alikuwa nayo hadi alipostaafu
tarehe 30 Juni 2002.
…/2
-2-
Marehemu Meja Jenerali
January Kisanko (Mstaafu) alifariki dunia tarehe 21 Machi, 2016 katika
Hospitali ya TMJ Dar es salaam. Ameacha Mke na Watoto. Mwili wa marehemu
unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 28 Machi, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi
katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika katika
makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, saa 10:00 jioni.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
MEJA JENERALI JANUARY KISANKO (MSTAAFU)
AMINA
No comments:
Post a Comment