Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, March 23, 2016

MWILI WA MAREHEMU SARAH DUMBA UMESAFIRISHWA LEO KUTOKA NJOMBE KUELEKEA DAR ESA SALAAM KWA MAZISHI



 KUSHOTO  NI ASKOFU ISSAYA JAPHET MENGELE NA KULIA NI MAKAMU ASKOFU DKT  GEOGE FIHAVANGU

 ASKOFU WA KKKT DAYOSISI YA KUSINI ISSAYA JAPHET MENGELE AMEONGOZA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU SARAH DUMBA KATIKA KANISA HILO


 MKUU WA WILAYA YA LUDEWA AKITOKA KUSOMA  HISTORIA YA MAREHEMU
 HII NDIYO PICHA  YA MAREHEMU SARAH DUMBA




 WAUMINI MBALIMBALI WA KIWA KANISANI HAPO KWAAJILI YA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA

 KATIBU MKUU KIONGOZI MSTAAFU FILEMON LUHANJO AKIWA NA VIONGOZI WA BENK YA CRDB AKIWEMO MENEJA WA BENK HIYO WAKIWA KWENYE MSIBA YA SARAH DUMBA




 HAPA MWILI UKIWASILI KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA ILEMBULA  UKIFIKA NYUMBANI KWAKE -IKULU NDOGO




Hatimaye Mwili Wa Aliyekuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Sarah Dumba  Umesafirishwa Leo Kuelekea  Dar Esalaam Kwaajili Ya  Mazishi   Ambapo  Kabla Ya Kuanza Safari Mwili Huo Umeagwa   Na Kupewa Heshima Za Mwisho   Na Waumini  Wa  Katisa La Kiinjili La Kiluthel Tanzania Dayosisi Ya Kusini  Pamoja Na Waumini Wa Makanisa Mengine.

Ibada Ya Kuuaga Mwili Wa Marehemu Sarah Dumba   Imeongozwa Na Askofu Wa Kanisa La Kiinjili La Kilutheli  Tanzania Dayosisi Ya Kusini  Issaya Japhet  Mengele  Na Kuhudhuriwa Na  Viongozi Wa Vyama Vya Siasa,Dini Na Serikali  Akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Filemon Luhanjo,  Barozi Mstaafu Godone Ngilangwa   Na Askofu Wa Kanisa Katholiki  Jimbo La Njombe Alfred Maluma.

Askofu Wa Kanisa La KKKT Dayosisi Ya Kusini Issaya Japhet Mengele Akiongoza Ibada Hiyo Amesema   Watumishi  Mbalimbali Wa Serikali Wanatakiwa Kurudisha Heshima Kwa Mungu Kama Alivyokuwa Akilitumikia Kanisa  Hilo Marehemu   Sarah Dumba Kwani Binadamu Hajui Siku Wala Saa Yakuchukuliwa Na Mungu.

Aidha Askofu  Mengele Amesema  Marehemu Sarah Dumba Ameonesha Mfano  Wa Kufanya Kazi Kwa Watumishi  Wengine Wa Serikali Na Wasiyo Wa Serikali Na Kwamba Mungu Hana Chama Na Wala  Cheo   Bali Binadamu Wote  Sawa  Na Njia  Ya Kuelekea Mbinguni  Ni Moja Huku Akisema Marehemu    Alionesha  Uadilifu Mkubwa  Kanisani.

Akizungumza  Na Uplands Fm Mara Baada Ya Kuuaga Mwili Wa Marehemu Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu  Filemon Luhanjo  Amesema Waandishi Wa Habari Wanatakiwa Kuiga Mfano Wa Marehemu Huyo Ambaye Ametunukia  Tuzo Mbalimbali  Kutokana Na Uandishi Wake Huku Akisema Amemfahamu Zaidi Wakati Marehemu Akihamasisha Wakulima Kulima Zao La Chai Ili Kuondoa Umasikini Miongoni Mwao.

Kwa Upande Wake Katibu Wa CCM Wilaya Ya Njombe Sadakat Kimatt  Amesema Enzi  Ya Uhai Wake  Sarah Dumba Alikijenga Chama Cha Mapinduzi  Katika Nyanja Mbalimbali Kanzia Kwenye Kamati Ya Siasa  Huku Akisema  Atakumbukwa Kwa  Kutumikia Chama Vizuri Kwa Kutekeleza Ilani Ya Chama Na Kusimamia Vizuri Halmashauri Tatu Na Kuhimiza Maendeleo.

Mwili Wa Marehemu  Sarah Dumba Ambaye Alikuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe  Unatarajia Kuzikwa Kigamboni Jijini Dar Es  Salaamu.

No comments:

Post a Comment