KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE PLODENSiANA PLOTAS AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI AKIWA OFISINI KWAKE
Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Limesema Limejipanga Kikamilifu Kudumisha Amani Na Utulivu Kwa Kukabiliana Na Uharifu Mbalimbali Utakaojitokeza Katika Kipindi Hiki Cha Skukuu Ya Pasaka Kwa Kuimarishila Ulinzi Katika Ofisi Za Serikali Na Za Watu Binafsi Bila Kusahau Maeneo Ya Nyumba Za Ibada.
Akizungumza Na Uplands Fm Radio Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Plodensiana Plotas Amewataka Wananchi Kusherekea Skukuu Kwa Amani Na Utulivu Pasipo Kuibua Vurugu Mbalimbali Zinazoweza Kuhatarisha Usalama Wa Eneo Husika Na Kutaka Serikali Za Mitaa Na Vijiji Kuonesha Ushirikiano Kwa Kutoa Taarifa.
Aidha Kamanda Plotas Amewataka Wamiliki Na Madereva Wa Vyombo Vya Moto Kuwa Makini Siku Ya Skukuu Wakiwa Barabarani Kwa Kuacha Kutumia Vileo Vya Aina Yoyote Ile Ambapo Jeshi La Polisi Limesema Halitasita Kuwachukulia Hatua Kali Za Kisheria Kwa Wale Wote Watakaokamatwa Kuhusika Wakiendesha Chombo Cha Moto Wakiwa Wamelewa Pombe.
Amesema Jamii Inatakiwa Kuondoa Imani Za Kufanya Matukio Ya Uharifu Msimu Wa Skukuu Kwa Kulewa,Kuvunja Nyumba Na Kufanya Uharifu Wa Kuiba Mali Ambapo Ametaka Wananchi Kupiga Simu Ya Kamanda Wa Polisi Ya 0754061979 Ili Jeshi La Polisi Liweze Kufika Eneo La Tukio Na Kufanikisha Kuimarisha Usalaama.
Kwa Upande Wake Baadhi Ya Wananchi Mjini Njombe Wameomba Watumiaji Wa Vyombo Vya Moto Kuwa Makini Wakiwa Barabarani Na Kusema Kuwa Vyombo Vinavyosimamia Usafirishaji Abiria Kuchunguza Baadhi Ya Madereva Ambao Wamekuwa Wakipandisha Nauli Msimu Wa Skukuu Na Wengine Kuchukua Abiria Wanaofika Mbali Na Wa Jirani Kuachwa.
No comments:
Post a Comment