WAZO LA WAZIRI WA ARDHI WILLIAM LUKUVI KUHUSIANA NA UWANJA ULIOMTOA MBWANA SAMATA KUFANYIWA KAZI
Mkuu wa
Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania Herieth Koka akimpongeza
Mbwana Samata kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji
wanaocheza soka la kulipwa Afrika, Wakati wa hafla ya kumpongeza
iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na wadau wengine wa Soka na kufanyika
katika hoteli ya Hyatty jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye
akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom
Tanzania Herieth Koka, wakati walipokutana katika hafla ya kumpongeza
Mbwana Samata aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa
ligi za Afrika. Kushoto ni Mchezaji bora wa Afrika 2015 Mbwana Samata.
Waziri
wa Nyumba na Makazi William Lukuvi akisalimiana na Mkuu wa Mauzo Kanda
ya Pwani wa Vodacom Tanzania Herieth Koka wakati wa hafla ya kumpongeza
Mbwana Samata kwa kutwa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji
wanaocheza soka la kulipwa afrika iliyofanyika katika hoteli ya Hyatty
jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ni mdhamini wa ligi kuu ya
soka Tanzania bara imesema kuwa bado inaufanyia kazi ushauri wa serikali
wa kuwa mmoja wa wafadhili wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa Mbagala
katika kumuenzi mwanasoka wa Tanzania Mbwana Samatta ambaye hivi
karibuni alitunukiwa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika.
Wakati
wa hafla ya wadau wa soka ya kumpongeza mwanasoka huyo juzi
iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam,mgeni wa
heshima kwenye hafla hiyo Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi,William
Lukuvi aliwataka wadau wa kuendeleza soka nchini ikiwemo kampuni ya
Vodacom inayofadhili ligi kuu kumuenzi Samatta kwa vitendo kutokana na
heshima aliyoiletea Tanzania ikiwemo kujenga uwanja aliokuwa anachezea
kabla ya kiwango chake kuwa kikubwa na kusajiliwa na vilabu
vinavyoshiriki ligi ya daraja la kwanza.
Mkuu
wa Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania,Herieth Koka amesema kuwa
ushauri huo wa serikali ni mzuri katika kumuenzi mwanasoka Samatta na
kampuni ya Vodacom itaufanyia kazi.
“Vodacom
ikiwa ni mdhamini mkuu wa ligi ya soka nchini tumefurahishwa na
mafanikio ya Samatta kwa kuwa moja ya dhamira ya kampuni yetu ni
kusaidia michezo hususani mchezo wa soka wa kuwa tunaamini kuwa bado
kuna fursa ya vijana wengi wa Tanzania maisha yao kuwa murua kupitia
michezo”.
Alisema
pia kuwa kampuni itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine
wa soka nchini kuhakikisha ligi kuu ya Vodacom inazidi kuwa bora ili
wapatikane wachezaji wengine wa kuitangaza Tanzania katika ramani ya
soka duniani kama alivyofanya Mbwana Samatta.
No comments:
Post a Comment