Sunday, January 3, 2016
WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI AINA YA MAWE WA KUTOKA MTAA WA SIDO MJINI NJOMBE WAMELAZIMIKA KWENDA OFISI YA MADINI MKOA KUPATA HATIMA YAO YA KUPEWA LESENI YA MACHIMBO
WACHIMBAJI HAO WAKIWA KATIKA OFISI ZA MADINI MKOA WA NJOMBE
MJIOLOJIA KUTOKA OFISI YA MADINI MKOA WA NJOMBE BWANA JOHN MAGANGA AMESEMA KWAKUWA HAWAJAFIKIA MWAFAKA WACHIMBAJI HAO NA SERIKALI YA MTAA YAKWAMBA NANI WAKUMILIKI LESENI HATAKIWI KUONEKANA MTU YEYOTE AKIGONGA MAWE ENEO HILO.
VIONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA SIDO WAKIRUDI NYUMBANI KWAO BAADA YA KUMALIZA KIKAO KATIKA OFISI ZA MADINI
Sakata La Wachimbaji Wadogo Wa Madini Aina Ya Mawe Wa Ganga Lyandefu Limeingia Dosari Baada Ya Wachimbaji Hao Kushindwa Kufikia Mwafaka Ya Nani Amiliki Leseni Ya Machimbo Ya Madini Kati Ya Serikali Ya Mtaa Na Kikundi Cha Wachimbaji Cha Jua Kali Hali Iliyosababisha Ofisi Ya Madini Kufungia Eneo Hilo Kuanzia Jana.
Akizungumza Na Waandishi Mjiolojia Kutoka Ofisi Ya Madini Mkoa Wa Njombe John Maganga Amesema Eneo Hilo La Machimbo Ya Ganga Lyandefu Halitakiwi Kuendelea Na Shughuli Za Uchimbaji Wa Madini Ya Mawe Kutokana Na Kikundi Cha Wachimbaji Wa Eneo Hilo Kushindwa Kufikia Mwafaka Na Serikali Ya Eneo Hilo Yakwamba Nani Amiliki Leseni Ya Machimbo Hayo.
Aidha Maganga Amesema Ofisi Ya Madini Haina Tatizo Na Mmiliki Wa Leseni Na Kwamba Mtu Yeyote Anaweza Kumiliki Isipokuwa Makubaliano Ya Wamiliki Wa Eneo La Madini Yanatakiwa Yawepo Ndipo Ofisi Hiyo Itowe Leseni Ambapo Wachimbaji Wa Madini Aina Ya Mawe Mtaa Wa Sido Kushindwa Kufikia Mwafaka Wanalazimika Kufungia Eneo Hilo Kwa Muda Usiyojulikana.
Wakizungumza Wakiwa Katika Ofisi Ya Madini Mkoa Wa Njombe Wanakikundi Cha Uchimbaji Madini Ya Mawe Jua Kali Cha Eneo La Ganga Lyandefu Katika Mtaa Wa Sido Wamesema Hawajaridhishwa Na Majibu Yaliotolewa Na Ofisi Ya Madini Pamoja Na Maamuzi Ya Serikali Ya Mtaa Wa Sido Ambapo Wameiomba Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Kuingilia Kati Sakata Hilo.
Wamesema Kutokana Na Maamuzi Hayo Wao Kama Wachimbaji Wa Eneo Hilo Wataendelea Na Shughuri Za Uchimbaji Kama Kawaida Hadi Serikali Ipeleke Jeshi La Polisi Liwapige Na Mabomu Lakini Wao Wataendelea Kufuatilia Ngazi Za Juu Kuanzia Diwani, Mkuu Wa Wilaya Na Mkuu Wa Mkoa .
Ray Mond Mbuligwe Ni Mwenyekiti Wa Kikundi Cha Wachimbaji Madini Ya Mawe Katika Eneo La Ganga Lyandefu Cha Jua Kali Amesema Kikao Hicho Hakija Zaa Matunda Kwani Wachimbaji Hao Wameshindwa Kuridhika Na Majibu Ya Kwenye Kikao Hicho.
Mtandao Huu Umemtafuta Kwa Njia Ya Simu Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Wa Sido Kutolea Ufafanuzi Juu Ya Hatima Ya Kikao Kilichofanyika Katika Ofisi Za Madini Mkoa Wa Njombe Kikiwa Na Lengo La Kuafikiana Juu Ya Machimbo Hayo Richard Bimbiga Amesema Hawezi Kuzungumza Chochote Kutokana Na Kuchoka Kwa Kuwa Alikuwa Kwenye Kikao Kwa Muda Mrefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment