SHEREHE MURWA YA JAMBO LEO YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2016
Baadhi
ya wafanyakazi wa Gazeti la Jambo Leo na familia zao, wakigongeana
glasi zenye vinywaji ikiwa ni ishara ya kutakiana heri wakati wa hafla
ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha ya Mwaka Mpya 2016, katika Mgahawa
wa City Sports Lounge, Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Jambo Leo na familia zao pamoja na wageni waalikwa
wakiburudika kwa muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika kwenye Mgahawa wa kisasa wa City Sports Lounge, katikati ya
Jiji la Dar es Salaam.
Mhariri
wa Michezo na Burudani wa Gazeti la Staa Spoti ambalo ni gazeti dada la
Jambo Leo, Zahoro Mlanzi akigawa ‘champagne’ kwa wafanyakazi wenzake
wakati wa hafla hiyo.
Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda (wa pili
kulia), akijadiliana jambo na wakurugenzi wa Kampuni za Jambo Concerpts
Tanzania Limited na Jambo Communication, Theophil Makunga (kushoto),
Benny Kisaka (wa pili kushoto) na Juma Pinto wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo, wakiwa na furaha wakati wa
hafla hiyo ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2016, Dar es
Salaam juzi. Kutoka Kushoto ni Stellah Kessy, Magendela Hamis, Salha
Mohamed, Celina Mathew, Suleiman Msuya na Edith Msuya.
Wakipata mlo wa usiku
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto), akimuelezea Mpiga Picha Mkuu wa
Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda kuwa wakati gazeti la Jambo Leo
lilipoanzishwa 2009, alikuwa mfanyakazi wa kwanza kujiunga na gazeti
hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto), akimuelezea Mhariri wa Habari wa
Gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe kuwa wakati gazeti la Jambo Leo
lilipoanzishwa 2009, alikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa kwanza kujiunga
na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto), akimuelezea Mwandishi Mwandamizi
wa Michezo na Burudani, Asha Kigundula kuwa wakati gazeti la Jambo Leo
lilipoanzishwa 2009, alikuwa miongoni mwa wafanyakazi wa mwanzo
kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
Mpigapicha Mkuu wa Jambo Leo na
magazeti mengine ya Staa Spoti na Jambo Brand Tanzania, Richard
Mwaikenda, akitoa shukrani wakati wa hafla hiyo/
Mfanyakazi Moi Dodo akiwa na wife wake
Champagne zikifunguliwa
Asha Kigundula akiwamiminia champagne wanahafla
Mwishehe na Kigundula wakikumbatiana kwa furaha
Sasa ni wakati wa kusakata muziki
Ni furaha tele
PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA
No comments:
Post a Comment