NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ATEMBELEA KITUO CHA JEMOLOJIA ARUSHA.
NAIBU
Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini,
Profesa James Mdoe ametembelea kituo cha Jemolojia jijini Arusha ambacho
hutoa mafunzo ya Jemolojia yanayojumuisha ukataji na uchongaji wa
madini ya vito na kuyaweka katika maumbile ya kuvutia.
Naibu
Katibu Mkuu alitembelea kituo hicho na Ofisi za Madini jijini Arusha ili
kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika pamoja na kuzungumza na
watumishi.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na
Madini, Profesa James Mdoe (wa Tatu kushoto) akiangalia mashine ya
ukataji madini iliyopo katika kituo cha Jemolojia jijini Arusha.Aliyevaa
shati jeupe ni Mratibu wa Kituo hicho, Mussa Shanyangi, wa kwanza
kushoto ni Afisa Madini Mkazi Ofisi ya Madini ya Merelani, Mhandisi
Henry Mditi na wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini nchini,
Mhandisi Ally Samaje.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na
Madini, Profesa James Mdoe (wa kwanza kulia) akiangalia mwamba
uliochongwa, kunakshiwa na kuwa katika umbo la mjusi wakati
alipotembelea Kituo cha Jemolojia jijini Arusha ambacho hutoa mafunzo
yanayojumuisha ukataji na uchongaji wa madini ya vito na kuyaweka katika
maumbile ya kuvutia. Wengine katika picha ni Afisa Madini Mkazi Ofisi
ya Madini ya Merelani Mhandisi Henry Mditi, (wa kwanza kushoto), Kaimu
Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje (wa pili kushoto) na wa
pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Uchumi na Biashara, Salim
Salim.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na
Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akionyeshwa moja ya mashine
zinazotumika katika Kituo cha Jemolojia jijini Arusha katika ukataji na
uchongaji wa madini ya vito na kuyaweka katika maumbile ya kuvutia.
Anayemwonyesha mashine hiyo ni Mratibu wa Kituo hicho, Mussa Shanyangi.
No comments:
Post a Comment