Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano aongea na Menejimenti ya iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi na kutembelea bandari
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo
wakati alipokutana na Menejimenti ya iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, na wakuu wa
Taasisi zilizo chini yake, katika Ofisi za Wizara hiyo leo asubuhi. Waziri
Mbarawa amewasisitiza Viongozi hao kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa kasi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kutoka
kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Edwin Ngonyani ( wa kwanza kutoka
kulia), wakimsikiliza Bi. Mkami Chacha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
wakati alipokuwa akiwaleza namna mashine ya Kukagua makontena inavyofanya kazi,
leo mchana wakati Mawaziri hao walipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA) kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania (TPA), Eng. Aloyce Matei akimwonyesha Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu) eneo itakapojengwa gati 13 na 14, wakati Waziri huyo
alipotembelea Mamlaka hiyo leo Mchana.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo
kwa wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali wanaofanya kazi katika kituo cha pamoja (one
stop center) katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakati alipowatembelea
leo Mchana. Waziri Mbarawa amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa
uadilifu.
No comments:
Post a Comment