HAPA WANANCHI WAPO KWENYE MKUTANO WA HADHARA ULIOWAKUTANISHA VIONGOZI WA KATA NA KIJIJI UKIONGOZWA NA DIWANI WA KATA HIYO VASCO MGUNDA
DIWANI WA KATA YA MFRIGA VASCO MGUNDA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI HICHO
DIWANI W AKATA YA MFRIGA VASCO MGUNDA ANAYEANDIKA MASWALI YA WANANCHI AKIWA AMESHIKA KICHWA
HAWA NI BAADHI TU YA WAJUMBE WA SERIKALI YA KIJIJI CHA ITAMBO KATA YA MFRIGA WILAYA YA NJOMBE
MTAALAMU WA KILIMU ONESMO MFUGALE AKITOA MAELEKEZO JUU YA PEMBEJEO ZA RUZUKU
Wananchi Wa Kijiji Cha Itambo Kata Ya Mfriga Wilayani Njombe Wameiomba Serikali Kuingilia Kati Tatizo La Kuuza Ardhi Katika Kijiji Hicho Ili Kuepukana Na Migogoro Ya Ardhi Yanayoweza Kujitokeza Hapo Baadaye Kutokana Na Maeneo Mengi Kununuliwa Na Wawekezaji Huku Maeneo Mengine Yakichukuliwa Kinyume Na Wamiliki Wake.
Wakizungumza Kwenye Mkutano Wa Hadhara Kijijini Hapo Wananchi Hao Wamesema Tatizo La Baadhi Yao Kuuza Ardhi Kiholela Linawapatia Mashaka Makubwa Kutokana Na Wengine Kukosa Kabisa Maeneo Ya Kulima Na Kuanza Kuvamia Maeneo Ya Watu Wengine Jambo Linaloweza Kusababisha Madhara Yatokanayo Na Migogoro Ya Ardhi.
Aidha Wananchi Hao Wamemuomba Diwani Wa Kata Ya Mfriga Kwa Kushirikiana Na Wataalamu Wa Halmashauri Kuweka Msharti Na Kufafanua Sheria Za Ardhi Kwa Kuelimisha Wananchi Juu Ya Matumizi Na Uthamani Wake Ili Na Kizazi Cha Baadaye Kiweze Kunufaika Na Rasilimali Ardhi.
Akizungumza Mbele Ya Wananchi Hao Diwani Wa Kata Ya Mfriga Ambaye Pia Ni Makamu Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Vasco Mgunda Amesimamisha Zoezi La Kuuza Maeneo Ya Ardhi Kiholela Katika Vijiji Vya Itambo Na Ikang'ssi Ambapo Amewataka Viongozi Wa Serikali Za Vijiji Hivyo Kutoruhusu Zoezi La Kuuza Maeneo Ili Kuepuka nMigogoro Ya Baadaye.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Itambo ...Amesema Serikali Yake Imekuwa Ikitoa Elimu Na Madhara Juu Ya Kuuzwa Kwa Ardhi Hiyo Lakini Bado Kuna Baadhi Ya Wananchi Wamekuwa Wakiendelea Kuuza Maeneo Yao Kwa Wawekezaji Pasipo Kutambua Madhara Yatakayojitokeza.
No comments:
Post a Comment