HAWA NI WACHIMBAJI WA MADINI WADOGOWADOGO WAKIWA KWENYE MKUTANO
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA SIDO RICHARD BIMBIGA AKIWA NA AFISA MADINI JOHN MAGANGA WAKITOA UFAFANUZI KWA WACHIMBAJI HAO.
BADO MIJADALA ILIKUWA INAENDELEA NA AFISA MADINI MKOA WA NJOMBE
WACHIMBAJI WA KIKUNDI CHA JUA KALI GANGA LYANDEFU WAKIWA KWENYE ENEO LAO LA MACHIMBO WAKISIKILIZA HOJA ZA VIONGOZI
MADINI AINA YA MAWE YANAYOPATIKANA ENEO LA MTAA WA SIDO
KOKOTO ZINAZOANDALIWA NA WACHIMBAJI HAO WADOGO NJOMBE
Afisa Madini Mkoa Wa Njombe John Maganga Amesema Wachimbaji Wadogo Wa Kikundi Cha Jua Kali Cha Ganga Lyandefu Kufikia Mwafaka Na Serikali Ya Mtaa Wa Sido Wa Kukata Leseni Za Madini Ili Waendelee Na Uchimbaji Huo Na Endapo Hawatafikia Mwafaka Na Serikali Ya Mtaa Huo Wataamulu Uchimbaji Huo Usitishwe.
Kauli Hiyo Ya Mtaalamu Wa Madini Mkoa Wa Njombe Bwana Maganga Imekuja Kutokana Na Mvutano Uliokuwepo Baina Ya Wataalamu Wa Madini,Serikali Ya Mtaa Wa Sido Na Wachimbaji Hao Ambao Wametaka Leseni Ya Machimbo Hayo Wakatiye Wenyewe Huku Serikali Ya Mtaa Ikitaka Ihusike Kukata Reseni Hiyo Kwa Kuwa Ndiye Msimamizi Wa Kwanza Wa Eneo Hilo.
Aidha Mtaalamu Wa Madini Huyo Bwana Maganga Amekili Kuwepo Kwa Mapungufu Yaliojitokeza Katika Kipindi Kilichopita Ya Kwamba Wachimbaji Hao Wapeleke Fedha Za Kulipia Leseni Moja Kwa Moja Ofisi Ya Madini Badala Ya Kuanzia Ofisi Ya Serikali Ya Mtaa Nakwamba Kwa Sasa Wanatakiwa Kukubaliana Na Serikali Ya Mtaa Ndipo Leseni Ziweze Kuwafikia .
Akizungumza Na Wachimbaji Wa Madini Hao Aina Ya Mawe Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mtaa Wa Sido Richard Bimbiga Amesema Wachimbaji Na Wataalamu Wa Madini Walikiuka Taratibu Za Kwenda Kukata Leseni Za Machimbo Hayo Ambapo Walitakiwa Kuishirikisha Serikali Ya Mtaa Ndipo Leseni Ya Eneo Hilo Iweze Kupatikana Kwa Urahisi KwaKuwa Ni Mali Ya Wakazi Wote Wa Sido .
Awali Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Wachimbaji Wa Madini Katika Eneo La Ganga Lyandefu Wamesema Hawako Tayari Kuiruhusu Serikali Ya Mtaa Ikate Leseni Ya Machimbo Hayo Kutokana Na Sababu Mbalimbali Ikiwemo Uongozi Uliomaliza Muda Wake Kuwadhulumu Pesa Za Machimbo Pamoja Na Kupata Tetesi Kwamba Kuna Muwekezaji Anataka Kumiliki Eneo Hilo.
Raymond Mbuligwe Ni Mwenyekiti Wa Kikundi Cha Wajasiliamali Cha Jua Kali Cha Ganga Lyandefu Amemuungana Na Wachimbaji Wengine Kwamba Leseni Inatakiwa Kukaa Na Wachimbaji Wenyewe Na Siyo Ofisi Ya Serikali Ya Mtaa Wa Sido Huku Akisema Eneo Hilo Mmiliki Siyo Serikali Bali Ni Wachimbaji Waliopo Eneo Hilo.
No comments:
Post a Comment