Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, December 27, 2015

Matamasha ya Halotel yafunika nchi nzima

 Wakazi wa Kahe wakifatilia tamasha la Halo Xmas katika Wilaya ya Kahe
 Msanii Msami akiburudisha wanakijiji wa Kahe katika tamasha la Halo Xmas
Msanii Shilole akiimba wakati wa tamasha la Halo Xmas lililofanyika wilaya ya Kahe.
 Wakazi wa Ruangwa wakifuatilia burudani ya tamasha la Halo Xmas lililofanyika katika uwanja shule ya msingi Likangala.
 
Matamasha ya Halotel yafunika nchi nzima
Matamasha ya Halo Xmass yaliyoandaliwa na kampuni ya Halotel katika mikoa mitano nchini yamefunika kwa kutoa burudani nzuri na kupata mahudhurio makubwa ya mashabiki.
Matamasha hayo ambayo yamefanyika wilaya za Tukuyu, Ruangwa, Moshi Vijijini, Chato pamoja na Mpwapwa, yamejumuisha wasanii wa bongo fleva pamoja na burudani nyingine kutoka kwa wasanii wa maeneo hayo.
Tamasha la Halo Christmass wilayani Tukuyu limefanyika katika uwanja wa Tandale na burudani imetolewa na wasanii Tundaman na Makomando.
Kwa upande wa Ruangwa, tamasha limefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Likangala, na kutumbuizwa na wasanii Amini pamoja na Matonya, wakati Mpwapwa tamasha limefanyika katika viwanja vya Mgambo likitumbuizwa na wasanii Madee na Malaika.
Wakazi wa Chato pia wamepata burudani ya kufunga mwaka katika viwanja vya Stand ya Zamani kutoka kwa msanii Shetta na Baraka Da Prince.
Moshi vijijini pia wamefurahia tamasha la Christmass kwa burudani kutoka kwa Shilole na Msami zilzofanyika katika viwanja vya Kaye.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo Moshi wameipongeza Halotel kwa kuwaandalia tamasha hilo wakisema hii ni mara ya kwanza burudani kubwa imefika kijijini kwao.
‘Makampuni mengi hupenda kufanya matamasha ya aina hii mijini, lakini kwa Halotel ni tofauti, kama namna huduma zao zilivyo za kipekee’ alisema Bi Halima Sanare, mkazi wa kijiji cha Kaye.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Halotel bwana Nguyen Thanh Quang, amesema matamasha hayo ya Halotel yalilenga kuwaleta watumiaji wa Halotel pamoja na kuwapa burudani ya kufunga mwaka.
‘Hii ni zawadi kwa watumiaji wa mtandao wetu na wateja wapya wanaotaka kujiunga na familia yetu ya Halotel, na ndio maana tunawafata katika maeneo yao yalipo’ alisema Quang.
Quang pia amewaahidi wateja wa Halotel kuwa mtandao wake unatarajia kuleta mabadiliko katika sekta ya mawasiliano nchini kwa kuwapa wateja wake zaidi ya huduma za simu.
Msanii Sheta akiimba na mtoto katika tamasha la Halo Xmas lililofanyika uwanja wa stendi ya zamani Chato.
 Madee akiburudisha mashabiki wa Mpwapwa katika uwanja wa Mgambo
 Msanii Matonya akiimba katika uwanja wa Ruangwa wakati wa tamasha la Halo Xmas.
 Baraka Da Prince akiimba wakati wa tamasha la Halo Xmas mjini Chato

No comments:

Post a Comment