Video
Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ akiwa na tuzo yake ya
Ijumaa Sexiest Girl 2015 baada ya kuwafunika Elizabeth Michael ‘Lulu’ na
Vanessa Mdee ‘Vee ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo
Mbagala- Zakhem jijini Dar.
Kidoa (katikati) akiwasalimia mashabiki baada ya kutangazwa mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2015.
...Akilia kwa furaha.
Kidoa akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Hamadombe Distributor, Fatuma Makame.
...Akibusu tuzo.
Akiwa
katika picha ya pamoja na mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na
kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor,
Amran Kaima (kulia).
Mwandishi
wetu
Fainali ya lile Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015 ilifanyika jana
ambapo Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ aliibuka
kidedea.
Kidoa alitangazwa mshindi kufuatia kupigiwa kura nyingi na wasomaji wa
Gazeti la Ijumaa hivyo kuwafunika wenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na
Vanessa Mdee ‘Vee Money’.
Akizungumza
na Risasi, mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya
uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima
alisema kuwa, ushindani ulikuwa mkubwa kwani wasanii wote walioshiriki
walikuwa wakali ile mbaya.
“Kidoa amefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupigiwa kura nyingi.
Atapokea tuzo, cheti pia atapewa ofa ya kutengeneza nywele kwenye saluni
ya Bulldozer iliyopo Kigamboni jijini Dar kwa miezi sita pamoja na
kufanyiwa shopping ya nguvu,” alisema Amran.
(PICHA NA RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA/GPL)
No comments:
Post a Comment