Friday, December 4, 2015
MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE WAAPISHWA RASMI JANA NA HAKIMU MKAZI WA MAHAKAMA YA WILAYA
HAKIMU WA MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE JOHN KAPOKORO AKIWAAPISHA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
HUYU NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAUL MALALA AKISOMA MAJINA YA MADIWANI WALIOCHAGULIWA KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA NJOMBE
Hakimu Mkazi Wa Mahakama Ya Wilaya Ya Njombe John Kapokoro Leo Amewaapisha Madiwani 17 Wa Halmashauri Hiyo Ambapo Madiwani Wateule Waliochaguliwa Na Wananchi Ni 12 Na Madiwani Wa Viti Maalumu Ni Watano Zoezi Ambalo Limefanyikia Katika Ukumbi Wa Halmashauri Ya Wilaya Hiyo.
Akizungumza Mara Baada Ya Kuwaapisha Madiwani Hao Hakimu Mkazi Wa Mahakama Ya Wilaya John Kapokoro Amewapongeza Kwa Hatua Ambayo Wamefikia Na Kutaka Kwenda Kutekeleza Majukumu Yao Katika Jamii Kwa Kufuata Misingi Na Maadili Ya Uongozi Bora Kulingana Na Kiapo Ambacho Wamepewa.
Akizungumza Mbele Ya Madiwani Hao Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Sarah Dumba Amesisitiza Madiwani Kuwa Waadilifu Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yao Kwa Kukusanya Mapato Kwa Wingi Ikiwa Ni Pamoja Na Kuziba Myanya Ambayo Imekuwa Ikisababisha Kuvuja Kwa Mapato Ya Halmashauri .
Katibu Tawala Msaidizi Serikali Za Mitaa Mkoa Wa Njombe Joseph Makinga Akizungumza Kwa Niaba Ya Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Ameiagiza Halmashauri Ya Wilaya Kwa Kushirikiana Na Madiwani Walioapishwa Kuhakikisha Wanatimiza Malengo Ya Ukusanyaji Mapato Ambapo Kwa Kipindi Cha Mwezi Julai Hadi Octoba Wameshindwa Kufikia Malengo.
Makinga Amesema Lengo La Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Katika Ukusanyaji Mapato Lilikuwa Ni Kufikia Bilioni Moja Na Milioni Mia 140 Lakini Halmashauri Hiyo Haijatimiza Hata Nusu Ya Kiasi Hicho Ambapo Kuanzia Mwezi Julai Hadi Octoba Imefanikiwa Kukusanya Kiasi Cha Zaidi Ya Shilingi Milioni 194.28 Sawa Na Asilimia 17 Tu Ya Makusanyo Yote.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Halmashauri Hiyo Na Makamu Wake Ambao Wamechaguliwa Kwenye Mkutano Wa Madiwani Valentino Hongori Wa Kata Ya Ikuna Na Vasco Mgunda Wa Kata Ya Mfriga Wameshukuru Kwa Kuwachagua Ili Waitumikiye Halmashauri Hiyo Na Kuomba Ushirikiano Katika Ukusanyaji Wa Mapato Hayo.
Awali Wakipokea Kiapo Madiwani Waliokuwepo Kwenye Mkutano Huo Wameahidi Kutumikia Na Kufanya Kazi Kwa Uadilifu Na Uaminifu Ikiwa Ni Pamoja Na Kufuatilia Mapato Ya Halmashauri Na Kuibua Vyanzo Vingine Kwaajili Ya Kukuza Uchumi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment