Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, December 10, 2015

KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITHABAHU AWA MGENI RASMI KWA NIABA YA RC KWENYE KILELE CHA UHURU JANA KIBENA.

KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE JACKSON SAITHABAHU AKIHOJI MATUMIZI  YA CHUMBA CHA CHANJO KIBENA


HIKI NI CHUMBA CHA KUHIFADHI CHANJO MKOA WA NJOMBE
DR.HAJI HUSSEIN MPAPAI MWENYE TRACKSUTI YA NJANO AKITETA JAMBO NA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI AGREY MTAMBO


DR.HAJI HUSSEIN MPAPAI AKIFANYA USAFI KATIKA HOSPITALI YA KIBENA

KATIBU TAWALA JACKSON SAITHABAHU AKIKWETUA NYASI ANA JEMBE KATIKA HOSPITALI YA KIBENA KATIKA  KILELE CHA MAADHIMISHO YA UHURU WA JAMHURI YA MUUNGANO.

DEREVA WA MTAALAMU WA TIBA MBADALA ZA ASILI HAJI HUSSEIN MPAPAI  NAYE AKIFANYA USAFI

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE BI.ILUMINATHA MWENDA AKIZUNGUMZA NA KATIBU TAWALA MSAIDIZI  SERIKALI ZA MITAA KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA JACKSON MAKINGA NA BAADHI YA WATUMISHI WENGINE.
AFISA AFYA MKOA WA NJOMBE  ALIYEVAA MIWANI MATHIAS GAMBISHI AKIMSIKILIZA  KATIBU TAWALA





KULIA NI AFISA AFYA MKOA WA NJOMBE MATHIAS GAMBISHI,WA PILI KUTOKA KULIA NI KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE AMBAYE ALIKUWA MGENI RASMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA KWENYE MAADHIMISHO HAYO,MWNYE  TRACK NYEUPE AINA YA SWETA NI DAKTARI MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

Watumishi Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Wametakiwa Kutenga Siku Maalumu Ya Kufanya Usafi Katika Hospitali Ya Kibena Kwa Kila Mwezi  Kwaajili Ya Kuboresha Mazingira Ya Hospitali Hiyo Huku Wananchi Kwa Kushirikiana Na Viongozi Wao Wakitakiwa Kufanya Usafi  Kila Siku Katika Maeneo Yao Wanayoishi.

Agizo Hilo Limetolewa Na Katibu Tawala Mkoa Wa Njombe Jackson Saithabahu Wakati Akiwa Mgeni Rasmi Kwenye Maadhimisho Ya Kilele Cha Uhuru Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Niaba Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe  Ambapo  Pia Ametaka  Watumishi Hao Kutenga Siku Nyingine Ya Kufanya Usafi Kando Ya Barabara Kuu Ya Kutoka Makambako  -Njombe.

Aidha  Saithabahu Amesema Wananchi Wanakiwa Kuepuka Utupaji Hovyo Wa Chupa Za Plasitiki Ambazo Wametumia Maji Na Sonda  Na Kutaka Viongozi Wa Serikali Za Vijiji Na Mitaa Kuhamasisha Utunzaji Wa Mazingira  Hususani Kwa Wasafiri  Wa Kwenye Mabasi  Na Wananchi Ambao Wana Tabia Ya Kutupa Hovyo Uchafu.

Katika Hatua Nyingine Katibu Tawala Huyo Jackson Saitabahu Amezindua Jengo La Chanjo Kwa Watoto Wenye Umri Chini Ya Miaka Mitano  Na Kuagiza Wakurugenzi Wa Halmashauri Kuhakikisha  Watoto Wote Wanapata Chanjo Katika Mkoa Wa Njombe Huku Watumishi Wa Idara Ya Afya Wanaohusika Na CHanjo Wakitakiwa Kuwa Makini Na Utunzaji Wa Jengo Na Vifaa Vyake.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mbunge Wa Jimbo La Njombe Mjini Edward Franz Mwalongo  Ametaka Wananchi Kubadili Tabia Na Kushiriki Kutunza Mazingira  Na Kukemea Yule Ambaye Atapatikana Anachafua Mazingira Kwa Kutupa  Chupa Za Maji Na Soda Kiholela Huku Akishuru Kwa Ushiriki Mkubwa Wa Wananchi Katika Maadhimisho Hayo.

Awali Akisoma Risala Mbele Ya Mgeni Rasmi Mratibu Wa Chanjo  Mkoa Wa Njombe Bi.Linda Chatila Amesema Fedha Iliyotolewa Na Shirika La UNISEF Kwaajili Ya Ukarabati Ni  Zaidi Ya Shiringi Milioni 52 Ambapo Gharama Ya Ukarabati Wa Jengo Ambalo Liliombewa Fedha Kwa Wafadhili Hao Na Ofisi Ya Mkoa Wa Njombe Kuwa Ni Zaidi Ya Shilingi Milioni 50.

Jumla Ya Watoto Elfu 26 Mia 582  Katika Mkoa Wa Njombe Na Akina Mama Wanaotarajia Kujifungua Laki Moja Na 68 Elfu Mia 409  Watanufaika Na Huduma Hiyo Ya Chanjo Katika Mkoa Wa Njombe.





No comments:

Post a Comment