Mkurungezi
Mkuu wa Marie Stopes
Tanzania, Anil Tambay akizugumza na wananchi (hawapo pichani) kwenye
bonanza la uzazi wa Mpango kwa vijana ambalo lilifanyika mwishoni mwa
wiki katika viwanja vya Mwembeyanga,Temeke jijini Dar.
Mgeni
rasmi Zukrah Mkwizu
akizungumuza na wananchi (hawapo pichani) kuhusiana na suala zima la
Uzazi wa Mpango,na kusisitiza kuwa uzazi wa mpangp ni silaha
imara ambayo vijana wanaweza kuitumia kupangilia maisha yao na kujikinga
dhidi
ya utoaji mimba usio salama na kulinda ndoto zao dhidi ya mimba
zisizotarajiwa.
Balozi
wa vijana wa Marie Stopes , Doreen Benne akifafanua jambo mbele ya
wakazi wa mji wa Temeke na viunga vyake waliofika kwenye kwenye Bonanza
la
Uzazi wa Mpango kwa Vijana lililofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya
viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam.
Mwanamuziki Barnabas Elias
'Barnaba akionesha umahili wake wa kulitawala jukwaa katika Bonanza la
Uzazi wa Mpango kwa Vijana Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam
Sehemu
Ya Wananchi Waliofika Katika Bonanza La
Uzazi Wa Mpango Kwa Vijana wakifuatilia yaliyokuwa yakijili kwenye
bonanza hilo ndani viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Jijini Dar Es
Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka , Globu ya jamii).
======= ======= ========
Wanamuziki
na Viongozi wa serikari ya Mkoa wanashirikiana na Marie Stppes Tanzania na zaidi
ya Vijana 1,000 kutoka vikundi mbalimbali vya vijana kuhamasisha upatikanaji wa
huduma za uzazi wa mpango, Mwembeyanga, Wilaya ya Temeke Leo.
Akiongea katika mkutano huu, Mkurungezi Mkuu wa Marie Stopes
Tanzania, Anil Tambay amesema, “Hiki ni kizazi kikubwa zaidi cha vijana katika
hisoria ya Tanzania, asilimia 54 ya Watanzania wapo chini ya umri wa Miaka 20.
Mafanikio yao yanamaanisha mafanikio ya Tanzania na mategemeo ya uchumi Imara
ambao kila mmoja wetu ataufurahia na kunufaika nao. Lakini wakati huo huo,
maisha na matarjio ya vijana yanaharibiwa – au wakati mwingine yanaishia pabaya
– kutokana na mimba zisizotarajiwa.”
Asilimia 44 ya wanawake Tanzania – karibu nusu yao – hupata
ujauzito wafrikiapo umri wa miaka 19. Huu huwa mwisho wa matarajio/ndoto ya
kielimu na taaluma au utoaji mimba usio salama, ambao idadi yao inakadiliwa
kuwa 1,500 kila mwaka kwa wanawake wanaoishi Tanzania – wengi wao wakiwa vijana
wa kike.
“Vijana wa kiume wanaathirika pia” Aliongeza Mr Tambay,
“Wengi wao hujikuta wanakuwa kin baba kabla hawajawa Tayari, hivyo hujikuta
wanaachana na mipago ya kwenda chuoni au chuo kikuu ili waweze kutafuta fedha
kwa ajili ya familia ambayo hawakuitarajia.”
Championi wengine wa upatikanaji wa huduma za Uzazi wa
Mpango kwa vijana kwenye tukio hili ni Bambo, Barnaba, Haika, Mwasiti, Nahreel
na Queen Darleen. Message inayotolewa ni kuwa,Uzazi wa Mpango ni silaha imara ambayo
vijana wanaweza kuitumia kupangilia maisha yao – kujikinga dhidi ya utoaji
mimba usio salama na kurinda ndoto zao dhidi ya mimba zisizotarajiwa.
“Leo tunawaambia vijana wachague Maisha mazuri kwa ajili
yao” Alielezea Mr Tambay,“Natunawaomba watu wote wenye madaraka – Manesi, Walimu
na Viongozi wa serikari – wasiwe vikwazo kwa upatikanaji wa huduma za uzazi wa
mpago kwa vijana badala yake wawaunge mkono na kwawashauri watumie
kiuwajibikaji. Napenda kumalizia kwa kusema, nawashukuru vijana wote waliofika hapa kushirikiana nasi.
Maria Stopes ipo hapa kwa ajili yenu na kwa ajili ya kwaunga
mkono kufanya maamuzi. Kama una ndoto, zilinde na jilinde kwa Uzazi wa Mpango.
No comments:
Post a Comment