MKUU wa
kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali,
Malima Nkilijiwando ambae pia ni mdau wa elimu ametimiza ahadi yake ya
kuinunulia Shule ya Sekondari ya Misitu iliyopo kata ya Kivule- Ukonga
jijini Dar es Salaam Kompyuta na mashine ya kutolea kopi pamoja na
kuchapisha.
Ahadi hiyo ameitimiza leo katika shule hiyo ikiwa aliahidi kipindi walipofanya mahafali ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu, Pantaleo Maghari amemshukuru Mkuu
wa kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za
Serikali, Malima Nkilijiwando kwa kuwa na moyo wa kusaidia elimu katika
shule hiyo kwani shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na tatizo la kompyuta
pamoja na mashine ya kuchapishia mitihani na kutolea kopi mitihani.
Shule hii
inakabiliwa na tatizo la uchache wa meza na viti vya kukalia wanafunzi,
mpaka sasa shule hii ya Sekondari ina wanafunzi 931 ikiwa ina viti na
meza 567 tuu. Alisema Maghari
Licha ya hivyo Maghari
alisema kuwa pia wanaupungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi, vyumba
vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo ikiwa mpaka sasa wanavymba vya
madara 12 tuu na matundu ya vyoo matundu 12 sita sita kwa wasichana na
wavulana ambavyo wanafunzi wanatumia kuanzia kidato cha Kwanza mpaka cha
nne ambavyo havikidhi mahitaji ya wanafunzi.
Aidha Maghari
alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa Elimu kuiangalia shule hiyo ya kata
ya Kivyule kwa jicho jingine ili wanafunzi waweze kupata elimu vile
inavyotakiwa.
Mkuu
wa kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za
Serikali, Malima Nkilijiwando akisaini kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili katika shule ya Sekondari ya Misitu iliyopo katika kata ya
Kivule-Ukonga jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari
ya Misitu, Pantaleo Maghari.
Mkuu wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando akikabidhi baadhi ya msaada wa Kompyuta na (nukushi) Printa katika shule
ya Sekondari ya Misitu iliyopo katika kata ya Kivule-Ukonga jijini Dar
es Salaam ikiwa ni ahadi aliyoitoka katika mahafari ya shule hiyo. Kulia
ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu, Pantaleo Maghari akipokea msaada huo leo shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando akimkabidhi kifaa cha kupunguza umeme Mkuu
wa shule ya Sekondari ya Misitu leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni
kutimiza ahadi yake aliyoiaidi siku ya mahafali ya kidato cha nne katika
shule ya Sekondari ya Misitu.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu akipokea baadhi ya vifaa vya Kompyuta kutoka kwa Mkuu
wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za
Serikali, Malima Nkilijiwando leo jijini Dar es Salaam . Nyuma ni
wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Misitu wakishuhudia mkuu wao wa shule
akipokea msaada huo ili kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakumba
walimu kwa kuwa walikuwa nanatumia pesa nyingi kwenda kutoa kopi nyingi
za mitihani sehemu nyingine, hivyo basi hawatafanya hivyo kutokana na
kutatuliwa changamoto hiyo.
No comments:
Post a Comment