Habari zilizotufikia zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani),
amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani.
Alikuwa na umri wa miaka 56.
Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na
kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku
ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya
maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko
Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki.
No comments:
Post a Comment