Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower( kushoto) akiendelea kutoa burudani ya nguvu huku msanii mwenzake Sony
Masamba akiendelea kuzirundi ngoma ndani ya kiota cha Escape One,
Mikocheni jijini Dar. Usikose leo siku ya Jumatano kwenye mkesha
wa EID maana kuna vitu vingi vipya.
Mwimbaji wa Bendi ya Skylight, Natasha pamoja na mwenzake Kasongo Junior haya ni Majembe mapya ya bend ya Skylight yenye uwezo mkubwa wa katika uimbaji.
Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake.
Sam Mapenzi pamoja (kulia) akiimba pamoja na Ashura Kitenge wakiendelea kuwakonga
nyoyo mashabiki wa Skylight Band waliofika siku ya Jumapili kwenye
kiota cha Escape One Mikocheni na leo sio ya kukosa njoo tukeshe pamoja
tukifurahi na mziki mzuri kutoka katika bendi hiyo.
Rapa
mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba huku mashabiki wa
bendi hiyo wakiserebuka kwa furaha na leo sio ya kukosa njoo na mwenzako
uje kuona vitu vipya kutka kwenye bendi hiyo.
Mwimbaji
wa Bendi ya Skylight, Natasha akiendelea kutuoa burudani kwa mashabiki
wao waliofika kwenye kiwanja cha Escape One kujionea burudani ya nguvu
kutoka katika bendi hiyo.
Msanii wa Bendi ya Skylight, Sony Masamba akiwafundisha mashabiki wao style mpya ya kucheza nyimbo za Bendi ya Skylight.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (katikati) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka Jumapili iliyopita katika kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
Msanii wa Bendi ya Skylight Ashura Kitenge akiimba kwa hisia kali mbele ya mashabiki i wa bendi hiyo(hawapo pichani) waliofika kwenye kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar kwa kuburudika na band hii.
Ilifika
time ya Nigeria Flavour Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa
na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu kwenye ngoma za
Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa
pili kutoka kushoto) pamoja na Sony Masamba.
Ilikuwa
noma sana siku ya Jumapili iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi
mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo Jumatano kwenye mkesha wa EID uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight ndani ya kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani ya kukata na shoka
Skylight
Band ni mwendo wa kutoa raha sana tukutane jumatano hii ndani ya kiota
cha Escape One, Mikocheni jijini Dar kwa kuburudika na band hii.
Mashabiki wa Bend ya Skylight wakiendelea kuserebuka na waimbaji wa bendi hiyo.
Sakata rhumba na Skylight band hapana chezea hatareee ukigusa lazima unase leo kwenye mkesha wa EID njoo wewe na rafiki yako
No comments:
Post a Comment