Kulia
ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori Tarime Mkoani Mara
akipokea Mahali ya binti wa Kaka yake kutoka kwa Mzee Samweli Chaha
Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu Tarime.
Na:George GB Pazzo
Baadhi
ya Watu wamekuwa wakiita ni Zawadi inayotolewa kwa Wazazi ama Walezi
pindi binti anapokuwa katika mipango ya kuolewa. Lakini kwa umaarufu
wake, watu wengi wamekuwa wakiita Mahali.
Kwa
siku za hivi karibuni kumekuwepo na majadiliano makali juu ya dhana
halisi ya Mahali. Hoja mbalimbali zimekuwa zikitolewa zikieleza kuwa
suala la Mahali kwa sasa si muhimu sana kama ilivyokuwa katika miaka ya
zamani hususani kwa baadhi ya makabila nchini ikiwemo kabila la Wakurya
wanaopatikana Mkoani Mara ambapo wazee wa kabila hilo walikuwa wakipokea
mamia ya ng’ombe kama mahali pindi mabinti zao walipokuwa katika
mipango ya kuolewa.
"Kwa
kabila la Wakurya bado suala la Mahali lina umuhimu mkubwa japo
kumekuwepo na mabadiliko kidogo. Zamani binti wa kikurya alipokuwa
akitaka kuolewa, Wazazi ama Walezi wake walikuwa wakipokea mamia ama
makumi ya ng’ombe kama sehemu ya mahali". Anaeleza mmoja wa wazee
Wilayani Tarime na kuongeza;
"Lakini
hivi sasa hali haiko hivyo tena kwani binti wa kikurya anaweza kuolewa
kwa Mahali chini ya ng’ombe 10 ama pesa kati ya Shilingi Laki Nne hadi
Milioni Moja na Laki Tano hii ikitegemea nafasi aliyo nayo binti. Mfano
Mahali inaweza kupanda kama binti ni msomi, Mrembo ama mwenye nidhamu na
maadili mema katika jamii".
Miongoni
mwa maoni yanayotolewa na baadhi ya wanaharakati wa kutetea haki za
binadamu yanakinzana na uhalali wa Mahali kwa misingi kwamba suala la
Mahali limekuwa halichukuliwi kama zawadi na watu wengi na badala yake
limekuwa likisababisha muoaji (Mme) kumnyanyasa muolewaji (Mke) kwa
minajili ya kwamba yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho juu ya mkewe kwa
kuwa tayari anakuwa amemlipia mahali ambapo hatua hiyo huondoa dhana
kuwa Mahali ni zawadi na kugeuka kuwa kumtolea binti Mahali ni sawa na
kumnunua ijapokuwa dhana hii inapingwa sana na watu wengi.
Hata
hivyo baadhi ya Wazee kutoka Kabila la Wakurya Wilayani Tarime
waliozungumza na Binagi Media Group wanaeleza kuwa bado suala la Mahali
lina umuhimu mkubwa sana hususani katika Kabila la hilo la Wakurya na
kwamba binti akitolewa mahali hueshimika katika jamii huku urafiki baina
ya pande zote mbili za familia kwa maana ya Mme na Mke ukiimarika
zaidi.
Je
wewe una mtazamo gani juu ya Mahali kwani licha ya kuchukuliwa kama
zawadi, baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa kumtolea binti Mahali ni
sawa na kumnunua. Wasiliana nasi kupitia nambari +255 (0) 757 43 26 94
au barua pepe binagimediagroup@gmail.com
Wa
pili Kulia waliokaa ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori
Tarime Mkoani Mara akipokea Mahali ya fedha kwa ajili ya kumuoza binti
wa Kaka yake aitwae Milika Daniel Marwa Binagi kutoka kwa Mzee Samweli
Chacha Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu Tarime.
Mahali Ikihesabiwa
Kushoto ni Professor Lloyd Binagi (Manamba) na Kulia ni Mzee Chaha Binagi wakihesabu pesa kwa jili ya Mahali ya binti yao
Baada
ya Mahali kukamilika hatua iliyofuata ni familia ya mme na mke kusaini
mkataba wa Makubaliano chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa
Mkataba ukisainiwa
Kulia
ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguti Rebu James Masoya akikabidhi
Mkataba wa Mahali na Mzee Maina (Kushoto) ikiwa ni upande wa binti
Kulia
ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguti Rebu James Masoya akikabidhi
Mkataba wa Mahali na Mzee Samwel Chacha Kebasa (Kushoto) ikiwa ni
upande wa mme
Sasa ni Msosi ambapo wageni upande wa binti wamekaribishwa na wenyeji wao upande wa mme
Sasa ni Msosi ambapo wageni upande wa binti wamekaribishwa na wenyeji wao upande wa mme
Wa kwanza kushoto waliosimama ndie Mkwe na hapo anatambulishwa Wazee
Picha ya Pamoja baina ya familia zote mbili kwa maana na mme na mke
Wazee wakibadilishana mawazo
Ndugu, jamaa na marafiki wakifurahia
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
Wazee upande wa binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya kuchukua Mahali kufikia tamati
Ndugu upande wa Binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya Mahali kukamilika
Ndugu upande wa Binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya Mahali kukamilika
Hatimae
wazee wakafika nyumbani na kufikisha habari njema kuwa Mahali
imechukuliwa na hapa wakaweka kumbukumbu ambapo Kutoka Kushoto ni Mzee
Maina Binagi, Milika Daniel Binagi na mwanae, Mzee Chacha Binagi, Leah
Daniel Binagi pamoja na Professor Lloyd Binagi
No comments:
Post a Comment