by SOLO Mazalla on August 6, 2015
Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishina Msaidizi wa Magereza (SACP) Annethy Laurent.
Mwili wa Marehemu Anneth ukiwasili katika kanisa katoliki parokiani Segerea tayari kwa misa takatifu ya kumuombea marehemu.
Mwili wa Marehemu Anneth ukiwasili
katika Kanisa Katoliki Parokiani Segerea. Walio mbele ni Pamela (mtoto
wa dada yake na Marehemu) na aliyebeba picha ni mtoto wa Pamela ( Mjukuu
wa Marehemu). Walioshika jeneza kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoa wa
Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Dk.Kato Rugainunura, kulia
ni Mkuu wa Kikosi Maalum Cha Magereza Kamishna Msaidizi wa Magereza
(ACP) Rajab Nyange
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati wa ibada ya kumuombea Marehemu.
Naibu Kamishna wa Magereza (DCP)
Edith Mallya akitoka salaam za Jeshi la Magereza kwa wafiwa kwa niaba ya
Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Lufunga akitoka
salaam za pole kwa wafiwa kwa niamba ya Kamati yake ambayo pia
aliongozana nayo katika msiba huo (hawaonekani pichani)
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama aliye pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Ally Lufunga(Mwenye
miwani) akitoa heshima za mwisho kwa marehemu. Wa pili ni Kamishna
Jenerali wa Magereza John Minja akifuatiwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini Eliakhim Maswi wakitoa salaam zao za
mwisho.
………………………………..
Na ASP Deodatus Kazinja-Makao Makuu ya Magereza
Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza (SACP) Anneth Balibusha Laurent umeagwa katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Segerea na kuzikwa katika makaburi ya Segerea
Jijini Dar es Salaam jana tarehe 06 Agosti, 2015.
SACP Anneth aliugua ghafla tarehe 29 Julai, 2015 Mkoani Shinyanga na kulazwa katika hospatali ya Mkoa huo lakini hali yake iliendelea kubadilika hivyo ikawalazimu kupelekwa katika hospitali ya Rufaa Bungando Mkoani Mwanza kwa matibabu zaidi ambapo jioni ya tarehe 30 Julai, 2015 alifariki dunia.
Akitoa salaam za Jeshi la Magereza katika msiba huo, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Malya kwa niamba ya Kamishna Jenerali wa Magereza alisema Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla limempoteza mtu muhimu aliyekuwa na sifa za pekee katika utendaji kazi wake lakini pia limempoteza katika umri wake mdogo.
Alitoa pole kwa familia, watumishi wa Jeshi la Magereza, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga na kwa wote walioguswa na msiba huo. Pia aliitolea mwito familia ya marehemu kuwa wavumilifu katika kipindi hiki kigumu lakini pia kuwa Ofisi yake itaendelea kushirikiana na familia hiyo kwa hali zote.
Aidha alisema kuwa Marehemu Anneth alikuwa miongoni mwa wanawake wachache wenye wadhifa wa Ukuu wa Magereza wa Mikoa hapa nchini ambapo jumla yao wako walikuwa wane tu na hivi sasa wamebaki watatu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Uslama wa Mkoa huo Ally Nassro Lufunga alisema Kamati yake imempoteza mtu muhimu sana kwani alikuwa ni kiungo katika shughuli zao mkoani lakini pia marehemu alikuwa ameleta mwamko mpya katika vikundi vya akina mama na akiwa kiongozi wa vikundi vya mazoezi nyakati za jioni baada ya kazi. RC Lufunga aliongozana na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama katika kumzika mjumbe mwenzao.
Kwa upande wake mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa niaba ya Katibu Mkuu alisema Wizara imempoteza mtendaji makini, kwamba wao kama wizara walimtazama Marehemu Aneth kwa kuzingatia umri, elimu , jinsia yake na cheo alichokuwa nacho kama mtu ambaye angekuja kusaidia huko mbeleni katika ule mpango wa kurithishana madaraka. “sisi kiutumishi pale wizarani ni pigo kubwa hatuna jinsi ni mipango ya Mungu itatubidi kujipanga upya, pole nyote” Alihitimisha
Marehemu Anneth Balibusha Laurent alizaliwa mwaka 1965 katika Kijiji cha Kibwera kata ya Kihanga Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Marehemu alijunga na Jeshi la Magereza tarehe 01 Septemba, 1994 akiwa ni Mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sanaa katika Uchumi na Mipango katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM)
SACP Anneth tangu kuajiriwa kwake amekuwa Afisa Mipango Makao Makuu ya Magereza hadi Octoba 2013 alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga.

No comments:
Post a Comment