Taarifa
iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde, inaeleza kuwa Mwenyekitu wa
Chama cha Wananchi -CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ametangaza
kujiuzulu wadhifa wake huo mbele ya Waandishi wa habari kwenye `hoteli
ya Peacock, Jijini Dar es salaam leo.
Prof. Lipumba amesema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kukiukwa kwa Katiba ya Chama chao.
TAARIFA KAMILI
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MWENYEKITI
wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba
amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa 5
asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mbele ya waandishi habari,Pro.Lipumba amesema ametafakari sana katika
kuendelea kuwa Mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.
Amesema
kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa
katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania katiba
itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lipumba
amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba
(UKAWA0 wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa
waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii
akilini.
Amesema
alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema
atang'atuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).
Amesema
amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia
kiasi hata kabambikiziwa kesi ya kufanya maandamano bila kibali.
Lipumba
amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaida, kufanya utafiti wa
maendeleo endelevu pamoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali
katika chama hicho.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akizungumza na Wandishi wa habari katika moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Peacok hotel jijini Dar leo kuhusiana na kung'atuka kwake rasmi Uenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida,ambapo Mh Lipumba ameeleza kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama hai na halali wa kawaida kwa sababu kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akitangaza kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha rasimu ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu
Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa
kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa
hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment