Mtangaza
nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM,Mh. January Makamba
akiagana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Bi Jesca Mambatavangu mara
baada ya January kusaini kitabu cha wageni katika ofisi za Chama.
Mchngaji
Kiwanga wa Iringa mjini akimkaribisha Mh. January Makamba na Mkewe
katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa. Mchngaji huyo alimwombea na kumpa
baraka zote za kugombea nafasi ya urais kupitia CCM.
Baadhi
ywa wanachama wa Waendesha Bodaboda waliojitokeza kumpokea na kumsapoti
Mh. January Makamba katika zoezi lake la kusaka wadhamini ndani ya
chama ili aweze kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya urais kupitia Chama
Cha Mapinduzi.
Mh.
January Makamba na Mkewe wakisalimiana na baadhi ya vijana na wanachama
wa CCM mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wiliya ya Iringa
Mjini.
Mh.
January Makamba na Mkewe wakiwapungia mkono baadhi ya vijana na
wanachama wa CCM waliofika kumsapoti mara baada ya kuwasili katika ofisi
za CCM wiliya ya Iringa Mjini.
Mh.
January Makamba akiweka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi za
CCM wilaya ya Iringa Mjini. Aliyesmama kulia kwake ni Katibu wa CCM
wilaya ya Iringa Mjini, Zongo Lobe Zongo na kushoto kwake ni mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, Abeid Kiponza.
Mh.
January Makamba akipunga Mkono kwa wanachama wa Iringa waliokuja
kumuunga mkono mara baada ya kutoka kuewka sahihi katika kitabu cha
wageni katika ofisi za CCM wilaya ya Iringa Mjini.
Badhi
ya vijana wa Iringa waliohuria katika viwanja vya ofisi ya CCM wilaya
ya Iringa Mjini wakimsikiliza Mh. January Makamba huku wakiwa wamebeba
mabango yenye ujumbe tofautitofauti.
Mh.
January Makamba na Mkewe wakiimba pamoja na wanachama wa CCM
waliojitokeza katika viwanja vya ofisi ya CCM wilaya ya Iringa Mjini
katika kumsapoti na kumdhamini kumuwezesha kushinda katika
kinyang'anyiro cha kupewa ridhaa ya kugombea urais kupita CCM.
Mh.
January Makamba akikabidhiwa fomu yenye majina ya wanachama
waliomdamini na Mwenyekiti wa CCM wilya, Abeid Kiponza. Fomu hiyo in
idadi ywa wanachama 630 waliojitokeza kumdhamini ikiwa ni kutoka wilaya
ya Iringa Mjini na Kilolo.
Mh.
January Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM wilaya ya
Iringa Mjini walijitokeza kumsapoti na kumdhamini. January amepata
sahihi 630 za wanachama wa CCM kumdhamini, idadi hiyo ni ya wilaya ya
Iringa Mjini na wilaya ya Kilolo. Picha Zote na Mpigapicha Wetu.
No comments:
Post a Comment