EMILIAN JOHN MSIGWA MTIA NIA YA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA JIMBO LA NJOMBE KUSINI
PEMBENI KABISA MWENYE SHATI NYEUPE NI MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM JIMBO LA NJOMBE KUSINI EDWARD MWALOGO AKISHUHUDIA MGOMBEA CHADEMA AKIRUDISHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA
MAANDAMANO YA CHADEMA KUMSINDIKIZA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NJOMBE KUSINI
OBADIA CHOGA NI KATIBU WA CHADEMA JIMBO LA KUSINI
WAGOMBEA WAKIRUDISHA FOMU NA KUSAINI KATIKA OFISI YA CHADEMA JIMBO
Mkurugenzi Wa Shule Za St Helliens Nchini Bwana Emilian Msigwa Leo Amerudisha Fomu Ya Kugombea Ubunge Jimbo La Njombe Kusini Kupitia Tiketi Ya Chadema Ambapo Ameomba Wananchi Kumpa Ushirikiano Ili Kuleta Mabadiliko Ya Kimaendeleo Kwa Wananchi.
Akizungumza Mara Baada Ya Kupokelewa Fomu Ya Kugombea Ubunge Bwana Emilian John Msigwa Amesema Kuwa Lengo Lake Kuu La Kugombea Ubunge Katika Jimbo La Njombe Kusini Ni Kutokana Na Kiongozi Ambaye Yupo Madarakani Kushindwa Kuwatembelea Waananchi Na Kutatua Changamoto Zinazowakabili.
Katika Hatua Nyingine Bwana Msigwa Amesema Kuwa Kiongozi Mwenye Sifa Ni Yule Anayekumbuka Kutatua Matatizo Ya Jimboni Kwake Ambapo Amezungumzia Changamoto Mbalimbali Zikiwemo Za Afya,Elimu Na Miundombinu Kuwa Itakwenda Kutatuliwa Kupitia Elimu Itakayotolewa Na Wataalamu Pamoja Na Yeye Akipita Kuwa Mbunge Kuihamasisha Serikali Iboresha Sekta Hizo.
Obadia Choga Ni Katibu Wa Chadema Jimbo La Njombe Kusini Amesema Kuwa JANA Ilikuwa Mwisho Kuchukua Na Kurejesha Fomu Za Kuwania Nafasi Mbalimbali Za Udiwani Na Ubunge Ambapo Ni Wagombea Tisa Tu wA uBUNGE Waliojitokeza Kurudisha Fomu Hizo Huku Akiwataka Wananchi Kuwaunga Mkono Ili Kuleta Mapinduzi Katika Jimbo La Njombe Kusini.
Bwana Choga Amesema Kuwa Kata Zote Wana Zaidi Ya Mgombea Mmoja Waliotia Nia Ya Kugombea Udiwani Katika Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Ambapo Hayo Yameelezwa Kuwa Ni Mafanikio Makubwa Na Kuwataka Wawategemee Kwani Wanakwenda Kuchagua Kiongozi Ambaye Atakuwa Msaada Kwa Wananchi Wote Wa Jimbo La Njombe Kusini.
No comments:
Post a Comment