Wafanyabiashara Wa Soko La Mbao Na Wamiliki Wa Magari Mbalimbali Yanayoelekea Mtaa Wa Kambalage Leo Wameandamana Hadi Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Ili Kushinikiza Uwezekano Wa Kutengeneza Barabara Hiyo Ambayo Imeshindwa Kupitisha Magari Ya Mizigo Na Abiria.
Wakiongea Na Uplands Fm Wafanyabiashara Na Wamiliki Wa Magari Hayo Wamesema Kuwa Wameshindwa Kusafirisha Mizigo Yao Ya Mbao Na Mali Nyingine Kwa Muda Wa Siku Tatu Kutokana Na Kuharibika Kwa Barabara Hiyo Ambapo Wameomba Serikali Iharakishe Kuwarekebishia Miundombinu Hiyo Ili Kufanikisha Kusafirisha Bidhaa Zao.
Aidha Wafanyabiashara Hao Wamesema Kutokana Na Kushindwa Kusafirisha Mizigo Yao Huenda Wakashindwa Kurejesha Mikopo Waliochukua Kwenye Taasisi Za Kifedha Huku Wakisema Wanashindwa Kuelewa Kwanini Serikali Inashindwa Kuboresha Miundombinu Hiyo Ikiwa Ushuru Wanalipa Shilingi Laki Tatu Kwa Kila Mfanyabiashara.
Wafanyabiashara Hao Walipofika Kwa Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Wamefanikiwa Kupewa Ushirikiano Ambapo Mkurugenzi Na Muhandis Wamefika Eneo La Tukio Na Kupeleka Mafuta Ya Gari Hilo La Barabara Ambalo Baada Ya Dakika Chache Liliharibika Na Kisha Wafanyabiashara WaKaamua Kufunga Barabara Ili Mgari Yasipite.
Katibu Wa Wafanyabiashara Wa Mbao Mkoa Wa Njombe Gipson Nyondo Amesema Kuwa Licha Ya Jitihada Za Kwenda Kwa Mkurugenzi Kuomba Mafuta Yapelekwe Kwenye Gari La Kulimia Barabara Hiyo Ambalo Limepakiwa Kwenye Eneo Hilo Korofi Tangu Jana Asubuhi Hakuna Mafanikio Walioyapata Baada Ya Gari Hilo Kuharibiuka.
Bwana Nyondo Amesema Kuwa Walipo Kwenda Kwa Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Walipelekewa Mafuta Rita Sitini Za Kujaza Kwenye Gari Hilo Ili Kurekebisha Eneo Hilo Bila Mafanikiwa Kutokana Na Kuharibika Kwake Ambapo Amesema Tatizo La Miundombinu Hiyo Limetoka Likiwasumbua Kwa Takribani Miezi Minne Sasa.
Mwenyekiti Wa Mtaa Wa Kambalange Bwana Braison Mgaya Amesema Amekuwa Akifika Katika Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kueleza Changamoto Zinazowakabili Lakini Hakuna Utekelezaji Wowote Kuhusiana Na Kutengeneza Miundo Mbinu Hiyo.
Kwa Upande Wake Kaimu Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Akizungumza Akiwa Eneo La Tukio Ambapo Barabara Inatakiwa Kurekebishwa Venance Msungu Akiwa Na Mhandis Wa Ujenzi Ibrahim Mkangara Wamesema Wanakwenda Kufuata Gari Lingine La Kwenda Kurekebisha Eneo Hilo Baada Ya Kuona Gari Lililokuwa Likitegemewa Kuharibika.
Bwana Msungu Amewasihi Wafanyabiashara Hao Kuwa Na Subira Wakati Halmashauri Ikilishughulikia Tatizo Hilo Mara Moja Ambapo Hadi Tunaingia Mitamboni Gari Hilo Lilikuwa Bado Halijafika Eneo La Tukio Ili Kurekebisha Barabara Hiyo Na Magari Yaweze Kupita.
No comments:
Post a Comment