1. Tarehe 1 Septemba 2014, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi Na. TR-G-14-039 kutoka
kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu kanuni ya
kukokotoa tozo za huduma ya kuchakata na kusafirisha Gesi Asilia, na
mapendekezo ya bei ya uchakataji na usafirishaji wa gesi asilia.
2. Kati
ya Septemba 2014 na Januari 2015, EWURA ilifanya uchambuzi wa kupitia
gharama za ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia, muundo wa mtaji
(capital structure) na faida ya mtaji, gharama za uendeshaji wa mradi,
pamoja na tozo iliyoombwa na TPDC.
3. Kwa mujibu wa ombi husika, TPDC waliiomba EWURA kuidhinisha vipengele vifuatavyo:
(a) kanuni ya kurekebisha tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia itumike kwa miaka 20 hadi mwaka 2034;
(b) tozo
kwa huduma ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia iwe Dola za Marekani
4.178 kwa uniti (MMBtu) kwa muda wa miaka mitatu ya kwanza;
(c) faida
kwenye mtaji ya asilimia kumi na nane (18%) na muundo wa mtaji wa
asilimia hamsini mkopo na asilimia hamsini fedha za TPDC (50:50); na
(d) mwezi
Septemba kila mwaka wa tatu utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo
kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa kwa EWURA.
4. Kwa
mujibu wa kifungu 19(2)(b) cha Sheria ya EWURA (Sura ya 414 ya Sheria
za Tanzania), tarehe 27 Novemba 2014, EWURA ilianza mchakato wa taftishi
kukusanya maoni na hoja za wadau kuhusu uhalali wa ombi
lililowasilishwa na TPDC. Wadau waliowasilisha maoni na hoja mbalimbali
ni Baraza la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (CCC), Baraza la
Ushauri la Serikali kuhusu Huduma za Nishati na Maji (GCC), Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Kampuni ya Saruji Tanzania (TPCC), PanAfrican
Energy Tanzania Limited, Songas Limited, Maurel & Prom, Wizara ya
Fedha, Wizara ya Maji, na Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, hoja za
wadau na ufafanuzi uliotolewa na TPDC vimezingatiwa na EWURA katika
kutoa uamuzi wa ombi hilo.
5. Tarehe
8 Januari na 6 Februari 2015, EWURA ilifanya mikutano na wadau wa
karibu (Exit Conference) ambapo EWURA ilisambaza rasimu ya Agizo la
EWURA (Draft Order) ili ijadiliwe na kupata maoni ya mwisho; na mkutano
huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa Wizara ya Nishati na Madini, Wizara
ya Maji, Wizara ya Fedha, CCC, GCC, TANESCO, TPDC, PAT, Songas, na TPCC.
Asasi zote hizo zilitoa maoni ya mwisho kwenye rasimu ya Agizo la
EWURA. Kwa ujumla, EWURA imezingatia maoni yaliyopatikana katika
mikutano hiyo na hatimaye kufikia maamuzi kwenye Ombi la TPDC.
6. Katika
kikao chake cha tarehe 19 Februari 2015, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA,
ilijadili Ombi la TPDC na kufikia maamuzi ya kipindi kifupi cha miezi
mitatu (Interim Tariff) ambacho TPDC itakitumia kukamilisha ujenzi na
kuwasilisha gharama halisi ambayo EWURA iliyahoji. Maamuzi yaliyotolewa
ni kama ifuatavyo:
(a) kanuni
ya kukokotoa tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia iliyoombwa
ilirekebishwa na kupitishwa ili itumike kwa miaka 20 kuanzia mwezi
Aprili 2015, na kurekebishwa kila baada ya miaka mitano;
| |
(b) gharama
za Mradi wa Bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara-Dar es
Salaam zilizopitishwa ni sawa na Dola za Marekani 1,331.51 milioni,
ambapo gharama hizi zitabaki hivyo hadi mwezi Juni 2015 ambapo gharama
halisi za mradi zitakapojulikana na kufungwa;
(c) gharama za uendeshaji zitakuwa sawa na Dola za Marekani 241.58 milioni kwa mwaka;
| |
(f) tozo
ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia italipwa kwa Shilingi za
Tanzania, kwa kiasi sawa na jumla ya Dola za Marekani 2.14 kwa uniti,
ambapo tozo ya kuchakata gesi asilia itakuwa Dola za Marekani 0.95 kwa
uniti. Kati ya hizo, na tozo la kusafirisha gesi asilia itakuwa Dola za
Marekani 1.19 kwa uniti. Tozo hizi zitatumika hadi hapo EWURA itakapotoa
agizo lingine baada ya kutathmini gharama halisi za mradi
zitakapojulikana na ujenzi kukamilika;
(g) endapo
EWURA haitatoa agizo jingine, tozo za kuchakata na kusafirisha gesi
asilia kama zinavyoonekana kwenye aya ya 6(f) hapo juu zitaendelea kwa
miaka mitatu (Aprili 2015 hadi Juni 2018);
(h) faida kwenye mtaji ya asilimia 4.58 na uwiano wa mtaji wa asilimia 75 fedha za mkopo na asilimia 25 fedha za TPDC (75:25); na
(i) mwezi
Septemba kila mwaka wa tatu, utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo
kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa kwa EWURA.
| |
7. Pamoja na maamuzi hayo hapo juu, TPDC wanaagizwa kutekeleza masharti yafuatayo:-
| |
(a) kuzingatia
kanuni za ushindani kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Manunuzi ya
Umma ya Mwaka 2011 (Public Procurement Act, 2011) na kuiarifu EWURA kila
TPDC inapofanya manunuzi ya thamani yanayozidi dola za Marekani 5
milioni.
(b) endapo
kuna ulazima wa kutumia utaratibu wingine kwa mujibu wa Sheria, ndani
ya siku thelathini (30) baada ya kuingia mikataba ya manunuzi TPDC
italazimika kutoa taarifa na kuwasilisha nakala za mikataba EWURA;
| |
(c) ndani
ya kipindi cha miezi kumi na miwili (12) baada ya Agizo la EWURA,
kuwasilisha EWURA, mpango wa uendelezaji wa miundombinu ya gesi asilia
(the Natural Gas Infrastructure Development Plan);
(d) ndani
ya kipindi cha miezi kumi na miwili (12) baada ya Agizo la
EWURA, kuwasilisha EWURA, mpango wa utumiaji wa miundombinu ya gesi
asilia iliyojengwa (the Natural Gas Infrastructure Utilisation Plan);
| |
(e) ndani
ya kipindi cha miezi kumi na miwili (12) tokea kuanza kwa Agizo la
EWURA, kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Wateja, ili kupima ufanisi katika
kutoa huduma za usambazaji wa gesi asilia na kushughulikia malalamiko ya
wateja.
(f) kuhakikisha
kwamba mfuko wa dhamana kwa ajili ya manunuzi ya gesi kutoka kwa
wawekezaji wenye visima vya gesi asilia unakuwa wa kiasi cha fedha
kisichopungua Shilingi 153 bilioni kila wakati kwa kipindi chote cha
mradi; Aidha;
(g) Kabla ya kuanza kutumika kwa Mkataba wa Huduma kwa Wateja, kuwasilisha mkataba huo EWURA kwa ajili ya kuupitisha; na
Agizo hili litaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 APRILI 2015
IMETOLEWA NAFELIX NGAMLAGOSI
MKURUGENZI MKUU
20 FEBRUARI 2015
| |
.png)
No comments:
Post a Comment