WATU watatu waliokuwa wamepakizana mishikaki wamekufa kwa kuteketea kwa moto mjini Iringa usiku huu baada ya usafiri aina ya pikipiki (Boda boda)waliyokuwa wakisafiri kutoka mjini Iringa kuelekea Nduli nje kidogo na mji wa Iringa kugongana na lori aina ya fusu na kupelekea pikipiki hiyo kuwaka moto.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 usiku huu wakati boda boda
hiyo ikiwa katika mwendo mkali kugongana na lori hilo ambalo pia
lilikuwa katika mwendo na kusababisha vifo hivyo .
Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na mtandao huu wa
www.matukiodaima.co.tz
wamesema kuwa
kijana mmoja ambae inasadikika ndie dereva wa boda boda hiyo
ametambuliwa kwa jina moja la Julius huku wengine wawili bado
kutambuliwa .
Kutokana na ajali hiyo mbali lori hilo upande wa mbele ngao yake
ilipinda huku eneo hilo la mbele likiharibika vibaya mfano wa
kugongana gari kwa gari na baada ya hapo pikipiki hiyo ilishika
moto na kuteketea yote pamoja na watu hao ambao miili yao
ilizimwa kwa mchanga na wasamaria wema.
Miili ya marehemu hayo imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha
Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa utambuzi zaidi
CHANZO: MATUKIO DAIMA
No comments:
Post a Comment