Tuesday, January 6, 2015
WATU WAWILI WAUWAWA NA WATU WASIYOFAHAMIKA MKOANI NJOMBE
Watu Wawili Wamefariki Kwa Kuuwawa Na Watu Wasiyofahamika Katika Matukio Mawili Tofauti Mkaoni Njombe Likiwemo La Mkazi Wa Kijiji Cha Ufwala Kata Ya Ilembula Wilayani Wanging'ombe Christopher Gerevas Maarufu Kwa Jina La Dava Aliyekutwa Amefariki Kwa Kukatwa Na Kitu Chenye Nja Kali.
Katika Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Iliyosainiwa Na Kamanda Wa Jeshi Hilo SACP Fulgence Ngonyani Imemtaja Christopher Gerevas Maarufu Kwa Jina La Dava Mwenye Umri Wa Miaka 32 Mkazi Wa Kijiji Cha Ufwala Na Mwili Wake Kukutwa Na Majeraha Yaliyochomwa Na Kitu Chenye Nja Kali Sehemu Za Kichwani Na Kwenye Jicho Na Kulazwa Kifudifudi Kwenye Mto Kiwogeka.
Amesema Kuwa Pembeni Mwa Mwili Wa Marehemu Huyo Kumekutwa Na Panga Ambapo Arifariki Januari 4 Mwaka Huu Wakati Akichunga Ng'ombe Polini Na Hakuna Ng'ombe Yeyote Aliyeibiwa Katika Tukio Hilo.
Katika Tukio Lingine Mkazi Wa Kijiji Cha Image Kata Ya Kidegembye Joseph Kinyamagoha Mwenye Umri Wa Miaka 54 Amekutwa Amefariki Dunia Nje Ya Nyumbani Kwake Kwa Kuuwawa Na Watu Wasiyofahamika Katika Tukio Lililotokea Januari 2 Mwaka Huu Majira Ya Saa Tano Usiku Kwa Kukatwa Na Kitu Chenye Nja Kali Kichwani Na Mkononi.
Kamanda Ngonyani Amesema Chanzo Cha Matukio Hayo Yote Bado Kinachunguzwa Kwa Kushirikiana Na Vikosi Vya Ulinzi Shirikishi Vya Maeneo Husika Ambako Matukio Hayo Yametokea Huku Likisema Hakuna Mtu Yeyote Anaeshikiliwa Kuhusika Na Matukio Hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment