Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, January 21, 2015

WAKULIMA WA CHAI LUPEMBE WILAYANI NJOMBEWAFANYA ZIARA YA LUNGWE KUJIFUNZA KILIMO CHA CHAI NA USHIRIKIANO BKATI YA MUWEKEZAJI NA WAKULIMA WADOGO WA CHAI LUNGWE


 PICHA YA PAMOJA YA WAKULIMA WADOGO WA CHAI LUPEMBE WAKIWA NA MKUU WA WILAYA BI.SARAH DUMBA NA WAKULIMA WADOGO WA CHAI LUNGWE





PICHA YA PAMOJA NA WAKULIMA HAO PAMOJA NA WAKULIMA WA LUNGWE




 WAWAKILISHI WA WAKULIMA WADOGO WA CHAI LUPEMBE WAKIWA NDANI YA SALE ZA WAFANYAKAZI WA CHAI LUNGWE WAKIJIANDAA KUINGIA KWENYE KIWANDA CHA LUNGWE

WAWAKILISHI WA WAKULIMA WA CHAI LUPEMBE WAKIWA NA BAADHI YA MADIWANI KATIKA KIWANDA CHA CHAI LUNGWE-JIJINI MBEYA
MTAALAMU WA KIWANDA CHA  CHAI LUNGWE  AKIWAELEKEZA NA KUWATEMBEZA WAKULIMA WADOGO WA LUPEMBE KIWANDANI HUMO








Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba Amewataka Wakulima Waliokwenda Kujifunza Kilimo cha Chai Lungwe Kwa Niaba Ya Wakulima Wengine Kuwa Chachu Ya Kuwaelimisha Wakukulima Wenzao Wa Lupembe Wakati Wakijianda Kuingia Ubia Na Kampuni Ya Chai Ya Kiwanda cha Ikanga Wilayani Njombe.

Akizungumza Na Baadhi Ya Wawakilishi Wa Wakulima Wa Lupembe Na Wakulima Wa Wilaya Ya Lungwe Mkoani Mbeya Mkuu Wa Wilaya Huyo Bi.Dumba Amesema Kuwa Mpango Huo Wa Kuwapeleka Wakulima Kujifunza Namna Walivyofanikiwa Kushirikiana Na Viongozi Wa Kiwanda Na Wakulima Wadogo Wa Zao La Chai Lungwe Utamsaidia Mkulima Wa Lupembe Kutumia Fursa Hiyo Kuboresha Kilimo Chao Kwa Manufaa Yao Na Muwekezaji.

Bi.Dumba Amesema Kuwa Kufuatia Ziara Hiyo Ya Kutembelea Wakulima Wadogo Wa Chai Lungwe Kumepanua Ufahamu Kwea Viongozi Wa Vyama Vya Wakulima Na Kwamba Wanatakiwa Kuacha Kuchanganya Siasa Na Kilimo Badala Yake WEatekeleza Majukumu Yao Ambapo Amesema Wakati Wakulima Wa Lupembe Wakielekea Kuingia Kupata Fursa Ya Kuingia Ubia  Na Muwekezaji Wa Kiwanda Cha Chai Ikanga  Ili Kushiriki Kukiendesha Kwa Pamoja Kutasaidia Wakulima Kunufaika Pamoja Na Muwekezaji Huyo.

Amesema Kuwa Wakulima Lupembe Sasa Wanatakiwa Kutumia Adhimu Ya Fursa Hiyo Katika Kuhakikisha Wanajikwamua Kiuchumi Kutokana Na Zao La Chai Nakwamba Kwa Sasa Lupembe Kumekuwa Na Amani Na Utulivu Tofauti Na Ilivyo Kuwa Hapo Awali Na Hivyo Wanatakiwa Kuendeleza Amani Hiyo.


Kwa Upande Wake Wawakilishi Wa Wakulima Wa Zao La Chai Wameshukuru Kampuni Ya Kiwanda Cha Ikanga Kwa Kuliona Hilo Nakwamba Semina Hiyo Imewanufaisha Kwa Kiasi Kikubwa Ambapo Wamesema Watakwenda Kuonesha Ushirikiano Mkubwa Kwa Viongozi Wa Kiwanda Ili Kufikia Malengo Yaliokusudiwa Na Kuingia Kwenye Mfumo Wa  Biashara Ya Fair Trade.

 

No comments:

Post a Comment