AFISA TARAFA YA NJOMBE MJINI LILIAN NYEMELE AKIZUNGUMZIA KATIBA INAYOPENDEKEZWA ITAKAVYOWAFIKIA WANANCHI
ASKOFU MENGELE AKISISITIZA JUU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWAMBA WATAUNGANA NA MAASKOFU WOTE KOTE NCHINI KUWAAMBIA WANANCHI WAIKATAE KATIBA INAYOPENDEKEZWA KUIPIGIA
Askofu Wa Kanisa La KKKT Dayosisi Ya Kusini Mkoani Njombe Issaya Japhet Mengele Amesema Endapo Serikali Haitafikisha Katiba Inayopendekezwa Kwa Wananchi Mapema Maaskofu Na Viongozi Wa Dini Wote Wataungana Nchi Nzima Kuwambia Wananchi Waikataye Katiba Hiyo Kwa Kuwa Hawajui Watakachokipigia Ifikapo April 30 Mwaka Huu.
Askofu Mengele Ametoa Kauli Hiyo Wakati Wa Zoezi La Uzinduzi Wa Shule Ya Sekondari Ya OSP Ruhuji Ambayo Imeanza Kusimamiwa Na KKKT Dayosisi Ya Kusini Kupitia Uongozi Wa Kidugala Seminari Tangu Januari Mwaka Huu.
Askofu Mengele Amesema Kuwa Viongozi Wa Dini Tanzania Walikutana Kwenye Mkutano Wa Maaskofu Na Viongozi Wengine Wa Dini Wakatoa Mapendekezo Yao Kwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwamba Kutokana Na Muda Kuwa Mchache Zoezi La Katiba Lifanyike Baada Ya Zoezi La Uchaguzi Lakini Wanashangaa Kuona Bado Kauli Yao Kupuuzwa.
Amesema Kuwa Uchaguzi Mkuu Wa Mwaka Huu Maaskofu Walipendekeza Serikali Iepuke Kutumia Siku Za Ibada Kuweka Siku Ya Uchaguzi Ambapo Itatakiwa Kuwekwa Siku Ya Jumatano Na Alhamisi Ama Juma La Kwanza La Mwezi Wa Kumi.
Afisa Tarafa Ya Njombe Mjini Bi.Lilian Nyemele Akizungumza Mbele Ya Waumini Wa KKKT Dayosisi Ya Kusini Amesema Serikali Inaendelea Na Zoezi La Kuhakikisha Wananchi Wanaipata Katiba Inayopendekezwa Kwa Muda Mwafaka Huku Akiwataka Wananchi Kutunza Amani Ya Nchi Iliyopo.
Mkuu Wa Shule Ya Sekondari OSP Ruhuji Bwana ...Akisoma Taarifa Ya Shule Hiyo Amesema Kuwa Pamoja Na Kuwepo Kwa Changamoto Za Ukosefu Wa Mabweni Na Nyumba Za Walimu Lakini Wanatarajia Kuanza Kuzitatua Changamoto Hizo Na Kuweza Kutoa Elimu Bora Kwa Wanafunzi Ambao Wanakwenda Kujiunga Shuleni Hapo.
Tulimtafuta Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba Ili Aweze Kuzungumzia Katiba Inayopendekezwa Kama Itawafikia Lini Wananchi Na Yeye Akawa Na Haya Kama Anavyotueleza Hapa
No comments:
Post a Comment