Monday, December 29, 2014
VIONGOZI WA MITAA LEO WAMEAPISHWA MJINI NJOMBE
MWANASHERIA MSAIDIZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE BAHATI KIKOTI
HAPA NI MTAA WA MGENDELA ZOEZI LA KUAPISHWA LILIFANYIKA LEO
MTAA WA NATIONAL HOUSING NDIYO HAPA
HAPA NI MTAA WA QWIVAHA WAKIPATA KIAPO WAJUMBE WA MTAA HUO
HAWA NI VIONGOZI WA MTAA WA BUGURUNI WAKIPATIWA KIAPO CHA KUANZA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MITAA YAO
HAPA NI MTAA WA SIDO WAKIWA KWENYE KUAPISHWA
HUYU NI MWENYEKITI WA MTAA WA KAMABALAGE
HAPA NI VIONGOZI WA MTAA WA KAMABALAGE WAKIAPISHWA NA HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO MJINI NJOMBE IZACK MLOWE ALIYEPO KWENYE MEZA KUU
WAJUMBE NA WENYEVITI WA MTAA WA IDUNDILANGA BAADA YA KUAPISHWA
MWANDISHI WA HABARI NA MTANGAZAJI WA UPLANDS FM RADIO MICHAEL NGILANGWA AKIZUNGUMZA NA WENYEVITI NA WAJUMBE WALIOAPISHWA KATIKA MTAA WA IDUNDILANGA AKTIKA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA.
Hakimu Wa Mahakama Ya Mwanzo Mjini Njombe Izack Mlowe Leo Anaendelea Na Zoezi La Kuwaapisha Viongozi Wa Serikali Za Mitaa Ambao Walichaguliwa Na Wananchi Katika Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Ulioofanyika Decemba 14 Mwaka Huu Nchini Kote Ambapo Hapo Jana Zoezi Hilo Lilifanyika Kwa Mitaa Ya Kata Ya Njombe Mjini.
Akizungumza Na Wenyeviti, Wajumbe Pamoja Na Baadhi Ya Wananchi Wakati Wa Kuanza Zoezi Hilo La Kuapisha Viongozi Wa Serikali Za Mitaa Kata Ya Njombe Mjini Hakimu Wa Mahakama Ya Mwanzo Izack Mlowe Amepongeza Kwa Kuchaguliwa Kwa Viongozi Hao Na Kwamba Mara Baada Ya Kuapishwa Viongozi Hao Wanatakiwa Kufuata Maadili Ya Uongozi .
Hakimu Huyo Wa Mahakama Ya Mwanzo Mlowe Amesema Kuwa Viapo Walivyopewa Ni Vya Kuanza Utekelezaji Rasmi Wa Majukumu Ya Serikali Za Mitaa Na Vijiji Kwa Kufuata Katiba Ya Nchi,Sheria Za Nchi ,Taratibu Za Nchi Na Maadili Ya Umma Ambapo Amesema Hategemei Kiongozi Yeyote Ambaye Atakiuka Kiapo Walichopewa.
Awali Akimkaribisha Hakimu Wa Mahakama Ya Mwanzo Mjini Njombe Izack Mlwe, Mwanasheria Msaidizi Wa Serikali Wa Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Bahati Kikoti Amesema Kuwa Lengo La Kuwaapisha Ni Kutokana Na Kuwepo Kwa Matakwa Ya Sheria Inayowataka Kutekeleza Zoezi La Kuapisha Viongozi Waliochaguliwa Ili Kuanza Kutekeleza Majukumu Yao.
Afisa Mtendaji Wa Kata Ya Njombe Mjini Bonasius Mwalongo Amesema Kuwa Baada Ya Halmashauri Ya Mji Wa Njombe Kufanya Zoezi La Kuwaapisha Viongozi Hao Wa Mitaa Halmashauri Hiyo Inatarajia Kwenda Kwa Awamu Nyingine Kuwapatia Semina Viongozi Hao Kwa Kuwa Halmashauri Kwa Sasa Haina Bajeti Ya Fedha Ya Kutolea Semina Hiyo Ambapo WanatakiwaKutekeleza Majukumu Yao Kusimamia Amani Na Utulivu.
Kwa Upande Wao Baadhi Ya Wajumbe Na Wenyeviti Walioapishwa Wamezungumzia Mipango Mikakati Ambayo Itawekwa Kuwa Ni Pamoja Na Kuanza Zoezi La Kuimarisha Ulinzi Shirikishi Pamoja Na Kutekeleza Miradi Ya Mitaa Kwa Kupata Maoni Kutoka Kwa Wananchi Kwa Kushirikiana Na Viongozi Wa Mitaa Jirani Pamoja Na Wananchi Wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment