Wednesday, December 31, 2014
MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA TOLLY MBWETTE AWAAGA WANACHUO NA UONGOZI WA CHUO HICHO KITUO CHA NJOMBE
HAWA NI WANACHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA KITUO CHA NJOMBE WAKISIKILIZA KWA MAKINI HOTUBA YA MGENI RASMI
MKURUGENZI WA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITUO CHA NJOMBE DKT SUSAN GWALEMA AKITOA TAARIFA YA CHUO HICHO KITUO CHA NJOMBE
WANACHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA KITUO CHA NJOMBE WAKIMKABIDHI ZAWADI MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU HIRIA PROFESA TOLLY MBWETTE
ALIYESHIKA KADI NI PROFESA TOLLY MBWETTE AKIONESHA ZAWADI ALIZOZAWADIWA NA WANACHUO.
MKUU WA MKOA WA NJOMBE DKT REHEMA NCHIMBI AKITOA HOTUBA AKIONGEA NA WANACHUO HAO
PICHA YA PAMOJA NA WANACHUO NA MGENI RASMI MKUU WA MKOA DKT REHEMA NCHIMBI NA PROFESA TOLLY MBWETTE
PICHA YA PAMOJA NA BAADHI YA WATUMISHI WA CHUO HICHO
Na Michael Ngilangwa-Njombe
Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amewaomba Wakurugenzi Wa Halmashauri Kuwatambua Walimu Wanaojiendeleza Kimasomo Kwa Kuwapatia Tuzo Wakati Wanapofanikiwa Ili Kujenga Mahusiano Na Ushawishi Kwa Walimu Wengine Kujiunga Na Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.
Akizungumza Na Wanachuo Kikuu Huria Cha Tanzania Kituo Cha Njombe Akiwa Mgeni Rasmi Wakati Wa Kumuaga Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Profesa Tolly Mbwette,Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi Amewataka Watumishi Wa Umma,Watu Binafsi Na Walimu Wa Shule Za Msingi Kutumia Fursa Hiyo Kuongeza Taaluma Zao.
Aidha Dkt Nchimbi Amewataka Walimu Wanaojiendeleza Na Kupata Elimu Za Juu Ikiwemo Deploma Hadi PHD Kubakia Katika Nafasi Zao Za Kazi Na Kwamba Kama Alikuwa Mwalimu Anatakiwa Kuendelea Kufundisha Kwenye Shule Zao Isipokuwa Kiwango Cha Mshahara Na Vyeo Vinatakiwa Kufikiliwa.
Dkt Nchimbi Amempongeza Profesa Huyo Kwa Kuanzisha Mufumo Wa Mahafali Kwa Wahitimu Wa Chuo Hicho Na Kwamba Mfumo Huo Unatakiwa Kuboreshwa Na Kutumiwa Kwa Nyanda Za Juu Kusini Ili Wahitimu Wakutane Kwaajili Ya Mahafari Na Kuhamasisha Wengine Kujiunga Na Chuo Hicho.
Akizungumza Mara Baada Ya Hotuba Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Muagwa Katika Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Profesa Tolly Mbwette Amesisitiza Viongozi Wa Chuo Wanaobakia Kuhimiza Matumizi YaTeHama Kwa Wanachuo Ambapo Amesema Katika Kipindi Cha Miaka Ijayo Matumizi Hayo Yatakuwa Ni Ya Razima Kwa Kila Mwanachuo.
Profesa Mbwette Amesema Kuwa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Kipo Kwenye Mazungumzo Na Wizara Ya Elimu Na Mafunzo Ili Kuangalia Uwezekana Wa Chuo Hicho Na Wizara Hiyo Kuwatafuta Walihitimu Wa Masomo Ya Sayansi Waliojiajiri Na Kuwapatia Mafunzo Maalumu Na Kuwapa Vyeti Vya Ualimu Kwaajili Ya Kuajiliwa Kwenye Shule Za Sekondari Hapa Nchini Kukuza Masomo Ya Sayansi Shuleni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment