JINA
la Rose Muhando ni mojawapo ya majina yanayofanya vizuri katika muziki
wa Injili barani Afrika hasa kutokana na uwezo wake jukwaani pindi
anapofikisha uinjilishaji kwa waamini na mashabiki mbalimbali.
Muhando
ni mzaliwa wa kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro,
Tanzania, Afrika Mashariki na ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa lugha
ya Kiswahili ambaye umahiri wake awapo jukwaani umefanikisha kutambulika
barani Afrika.
Rose
atakayepanda jukwaani kuanzia Desemba 25, Agosti 3 mwaka huu alizindua
albamu yake Kamata Pindo la Yesu yenye nyimbo za ‘Facebook’, ‘Bwana
Niongoze’, ‘Wewe Waweza’, ‘Usiniache’, ‘Nibariki na Mimi’, ‘Usivunjike
Moyo’ na ‘Kwema’.
Awali
Rose kabla hajawa Mkristo alikuwa Muislam na ni mama wa watoto watatu.
Alimpokea Yesu Kristo pale alipokuwa anaumwa na yuko kitandani akiwa na
umri wa miaka 9, aliugua kwa muda wa miaka mitatu na baadae alipona na
kubadili dini na kuwa Mkristo.Rose
alizama kwenye muziki katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa
Kwaya katika kwaya ya Dodoma St. Mary’s katika kanisa la Kianglikana la
Chimuli.
Januari
31 mwaka 2005, Rose Muhando alizawadiwa tuzo ya Mtunzi bora wa nyimbo
za Injili, Mwimbaji Bora na albamu Bora ya Mwaka. Tuzo hizo zilitolewa
katika Tamasha Tanzania Gospel Music Awards, 2004.Desemba
mwaka 2005 alihudhuria katika tamasha la Nyimbo za Injili katika
kusaidia kuchangia kwa watoto na wajane Dar es Salaam ambapo alitekeleza
ipasavyo uchangiaji huo.
Februari
2011, Rose Muhando alisaini mkataba na Mult Album Recording Deal na
Kampuni ya Sony Music ya Afrika Kusini. Kusaini huko kulitangazwa katika
mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Tanzania na hiyo ni mara
ya kwanza kufanyika Afrika Mashariki.
Baadhi ya albamu za Rose Muhando ni:
1. Mteule uwe macho, 2004
2. Kitimutimu, 2005
3. Jipange sawasawa, 2008
4.Utamu wa Yesu 2012
4.Kamata Pindo la Yesu 2014
Tuzo alizopata
2005 -Tanzania Music Awards: Mwimbaji Bora wa Kike Nyimbo za Dini (“Mteule uwe macho”)
2009 - Mwimbaji Bora wa Nyimbo za Injili
2008- Alitunukiwa tuzo nchini Kenya ya Mwimbaji Bora wa Injili Afrika
Amewahi kuzawadiwa kitita cha Sh200,000 na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
No comments:
Post a Comment