Katibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Njombe akizungumza na vyombo vya habari.
Na James Festo, Njombe.
KATIBU wa chama cha Mapinduzi Mkoani Njombe Hosea Mpagike ameviomba vyama vya siasa Nchini kuacha kutumia nguvu kubwa katika chaguzi mbalimbali na badala yake kuelimisha jamii juu ya wanachotarajia
kufanya baada ya kupata nafasi.
Mpagike amesema kuwa " tunatakiwa kufanya kampeni za kistaarabu kwa kujenga hoja atafanya nini baada ya kuchaguliwa lakini sio hoja za kuchafua mgombea niwaombe sana suala la siasa ni la kidemokrasia kila mmoja anahaki lakini sio ya kuchafua mwingine"
Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya uchaguzi kwa upande wa chama chake kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulionekana kukumbwa na changamoto nyingi zikiwamo za kutoonekana kwa majina na kusababisha wapiga kura kuchukua mda mrefu wakati wa kupiga kura na kuelezea hofu yake juu ya watu kupigwa kura mara mbili.
Aliiomba Ofisi ya Waziri mkuu endapo itaendelea kusimamia uchaguzi huo wahakikishe wanaweka utaratibu wa kuchapishwa kwa majina sambamba nakutatua changamoto zote zilizojitokeza katika vituo vingi nchini.

" Katika uchaguzi huu tumekuta malalamiko mengi ambayo walikuwa majina yao hawayaoni nje na katika karatasi ya msimamizi ndani walikuwa wanayakuta" alisema Mpagike.
Akizungumzia matokeo ya uchaguzi kwa mkoa wa Njombe alisema kuwa Wilaya ya Njombe alisema kuwa kuna vijiji 108 na vijiji saba havikufanya uchaguzi na kati ya vijiji vlivyofanikiwa kufanya uchaguzi CCM ilipata vijiji 94 sawa na asilimia 93 na CHADEMA kimechukua vijiji 8 sawa na asilinia 7.44.
Alisema kuwa katika uchaguzi uliofanyika kwenye mitaa iliyopo Halmashauri ya Mji wa Njombe na Makambako zenye jumla ya mitaa 82 ambapo CCM ilichukua juma la mitaa 54 sawa na asilimia 66 ambapo CHADEMA imechukua mitaa 28 ambapo ni sawa na aslimia 34 na chama cha NCCR Mageuzi imechukua kijiji kimoja.
Aliongeza kuwa katika halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe kulikuwa na vijiji kulikuwana vijiji 108 ambapo vijiji 4 havikufanya uchaguzi na katika CCM ilichukua vijiji 102 sawa na asilimia 98.1 na chadema ilichukua vijiji 2 sawa na asilimia 1.9.
Katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa Chama cha CCM kilifanikiwa kuchukua jumla ya vijiji 77 ambapo vijiji 4 havikufanya uchaguzi na kuwa CCM ilichukua vijiji 64 sawa na asilinia 97 na Chadema imechuku vijiji 9
sawa na asilimia 3.
Aidha Mpagike alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya makete CCM ilifanikiwa kuchukua viti 46 huku CHADEMA ikichukua vijiji nane sawa na asilimia 68.
Mpagike alitoa wito kwa watu ambao wamekuwa wakizani kuwa uchaguzi sio sehemu za kunyeshana nguvu na kuvitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya kuwapakazia wagombea wetu kwa kuaandaa hoja za kuwatumu.
No comments:
Post a Comment