Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa Mazingira
wa Dunia (Cop20) (hawapo pichani) alipokuwa akiwahutubia leo Desemba 11,
2014. Katikati ni Waziri wa Mazingira wa Sudan, (kushoto) ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Wataalam ya Afrika katika masuala ya Majadiliano ya
Mabadiliko ya Tabianchi kutoka nchini Sudan, Nagmeldin El-Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa Mazingira
wa Dunia (Cop20) (hawapo pichani) alipokuwa akiwahutubia leo Desemba
11, 2014. katika mkutano wa Mazingira wa Dunia unaoendelea Jijini Lima,
nchini Peru.Katikati ni Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,
Tanzania, Dkt. Binilith Mahenge.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam ya Afrika
katika masuala ya Majadiliano ya Mabadiliko ya Tabianchi kutoka nchini
Sudan, Nagmeldin El-Hassan, wakati alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa
mikutano kwa ajili ya kuzungumza na wawakilishi wa Afrika katika mkutano
wa Mazingira Duniani (Cop20) unaoendelea jijini Lima, nchini Peru.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na baadhi ya wawakilishi wa Afrika katika mkutano wa
Mazingira wa Dunia (Cop20) baada ya kuwahutubia leo Desemba 11, 2014,
katika Mkutano wa Mazingira Duniani na majadiliano kuhusu Mabadiliko ya
Tabianchi, unaoendelea jijini Lima, nchini Peru.
Sehemu ya Wawakilishi wa nchi za Afrika katika mkutano wa Mazingira
Duniani, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati
akiwahutubia leo, Desemba 11, 2014, mkutano wa Mazingira Duniani
(Cop20) unaoendelea jijini Lima, nchini Peru. Picha na OMR
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
AHUTUBIA WAWAKILISHI WA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA MAZINGIRA DUNIANI
(COP20) JIJINI LIMA, PERUDESEMBA 11, 2014
Mheshimiwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal jana Desemba 10, 2014, amewahutubia wawakilishi wa Afrika katika
Mkutano wa Mazingira Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, nchini
Peru. Mheshimiwa Makamu wa Rais anahudhuria mkutano huu akimuwakilisha
Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Kiongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali
kutoka Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi. Mkutano huo wa jana
ulikuwa na dhima ya Afrika baada ya mwaka 2015: Makubaliano Mapya kuhusu
Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Awali Mheshimiwa
Dkt. Bilal aliwaambia wawakilishi wa Afrika katika mkutano uliojumuisha
Mawaziri wa Afrika wanaoshughulikia masuala ya Mazingira katika nchi zao
kuwa, Afrika licha ya unyonge wake bado inalo jukumu la kusimama kidete
katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na ili kufanikiwa katika
jambo hilo ni muhimu kwa Bara hili kuwa na sauti ya pamoja.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa, Bara la Afrika lina kila sababu
ya kuwa na mipango yake ambayo itatumika kushirikisha nchi za nje ya
Afrika ili kwa pamoja Dunia iweze kuwa na kauli inayofanana yenye
kulenga kukabiliana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya Tabia Nchi
licha ya kuwepo tofauti za kimaendeleo kati ya Afrika na nchi za mabara
mengine.
Awali akizungumza kabla ya Mheshimiwa
Makamu wa Rais, Waziri wa Mazingira wa Sudan ambaye ni Mwenyekiti wa
kundi hili la Afrika Dkt. Hassan Albdelgadir Hillal alisema, kundi la
Afrika linapongeza uongozi wa Tanzania kupitia kwa Rais Jakaya Kikwete
kwa namna unavyosimamia agenda hizi za mabadiliko ya Tabia Nchi na
kusimamia upatikanaji wa sauti moja kutoka kwa nchi za Afrika. Dkt.
Abdelgadir aliendelea kusema kuwa, Afrika inatakiwa kutumia mkutano huu
wa Lima kwa umakini ili kuhakikisha mipango inayofikiwa inapata
kutambulika na kuonekana mwakani wakati mkutano kama huu utakapofanyika
jijini Paris.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Binilith Mahenge ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Mawaziri wa Mazingira kwa nchi za Afrika yeye alibainisha
kuwa, viongozi wa nchi za Afrika wamekuwa mstari wa mbele kabisa
kuhakikisha kuwa Afrika inasikika na kwamba anatarajia ushirikiano
katika ngazi ya Mawaziri kuendelea hata pale atakapokuwa anakabidhi
nafasi hiyo kwa Waziri wa Mazingira wa Misri.
Katika
mkutano mwingine ambao pia ulikuwa mwendelezo wa Siku ya Afrika katika
COP20, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alisisitiza kuwa Afrika
inatakiwa kuhakikisha vijana na akina mama wanakuwa mstari wa mbele
katika kukabiliana na hali hii ya mabadiliko ya tabia nchi.
“Makundi
haya ni muhimu sana kwa kuwa ndiyo yanayohusika moja kwa moja na
shughuli za kila siku. Hatutaweza kufanikiwa kama tutayaacha makundi
haya nyuma,” alisema Mheshimiwa Makamu wa Rais katika Mkutano huo ambao
pia ulihutubiwa na Dkt. Fatima Denton, Mkurugenzi wa Harakati Maalum
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kamishenbi ya Uchumi kwqa Afrika
(UNECA).
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Lima, Peru
No comments:
Post a Comment