Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss)
uliofanyika katika ukumbi wa St. Peter's jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE -
Saccoss), mama Anna Matinde na Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal.
Picha zote na Cathbert Angelp Kajuna wa Kajunason Blog.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akishirikiana na Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikabidhiwa zawadi kwa mchango wake anaoutoa katika jamii.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akiongea machache.
Mwenyekiti
wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama
Anna Matinde alisema "Tumeanzisha Saccos hii ili kupambana na changamoto
za upataji wa mikopo kwa riba kubwa na kuwajengea watanzania tabia ya
kuweka akiba.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikagua miradi mbali mbali
inayoendeshwa na akina mama wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (
TASWE - Saccoss) wakati wa uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa St.
Peter's jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akionyeshwa jiko la kisasa
linalopunguza matumizi. Pembeni kwake ni Balozi Mdogo wa India,
Baluinder Humpal katikati wakiongozwa na mwenyeji wao Mwenyekiti
wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna
Matinde.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi leo Disemba 10, 2014
amezindua Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss)
itakayowawezesha watanzania na wanachama kuweka akiba, kukopa na kununua
hisa kwaajili ya kupata mitaji ya kuboresha shughuli zao za kijamii na
kiuchumi.
Akiongea
wakati wa uzinduzi Dk. Mengi aliwataka wanachama watumie fursa hii
kupata mikopo kwaajili ya kutanua biashara zao, lakini pia wahakikishe
wamejipanga mathubuti na kujiwekea malengo endelevu ambayo yataleta tija
katika maendeleo yao.
"Nanawatia moyo wote, na pia ninapenda kuwapongeza sana na nawatakia kila lakheri" Alisema Mengi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (
TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde alisema "Tumeanzisha Saccos hii
ili kupambana na changamoto za upataji wa mikopo kwa riba kubwa na
kuwajengea watanzania tabia ya kuweka akiba. Mpaka sasa tuna wanachama
zaidi ya 200 hapa Dar es Salaam na tumejipanga kutanua wigo na kufungua
matawi zaidi Kanda ya Kaskazini, mikoa ya Dodoma, Mtwara, Lindi, Mwanza
hadi ifikapo mwezi wa tatu mwakani.
Lakini
pia ipo miradi tuliyonayo yenye lengo la kuinua na kukuza chama hiki
cha saccoss na kunufaisha wanachama wake.Ofisi zetu ziko Oysterbay, Dar
es Salaam hivyo nawakaribisha wanachama wapya kujiunga
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa email annamatinde@gmail.com au 0754692994.
No comments:
Post a Comment