DODOMA
Baada ya Mvutano Mkubwa wa Namna ya Kuwawajibisha Viongozi Mbalimbali Wakiwemo Mawaziri Waliohusika na Tuhuma Nzito ya Sakata la Wizi wa Fedha Katika Akunti ya Tegeta Escrow Hii Leo Wabunge wa Vyama Vyote Wamekubaliana Kufanya Maamuzi Magumu Kwa Kuishauri Mamlaka ya Uteuzi Kutengua Uteuzi Wao.
Katika Mvutano Huo Ulioanza Tangu Novemba 28 Mwaka Huu Baada ya Waziri Wa Nishati ya Madini Kuwasilisha Utetezi Wake,Huku Kwa Siku ya Leo Bunge Likilazimika Kuahirishwa Mara Tatu Bila Kupata Suluhu Kutokana na Kigugumizi Kikubwa Cha Kuhofia Kiingilia Muhimili Mwingine Bunge Limeazimia Mawaziri Wawili Pamoja na Watumishi Wawili na Bodi ya Shirika la Umeme Tanesco Kuwajibishwa.
Akiwasilisha Maazimio ya Bunge Hilo Baada ya Maazimio ya Awali ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kutenguliwa,Mwenyekiti wa Kamati Hiyo Bwana Zitto Kabwe Amesema Bunge Hilo Limeazimia Waziri wa Nishati na Madini,Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Pamoja na Bodi ya TANESCO Kuwajibishwa Kwa Kuishauri Mamlaka ya Uteuzi Kutengua Uteuzi Wao.
Aidha Zitto Amesema Kuwa Bunge Hilo Pia Limeshauri Uchunguzi Ufanyike na Kutoa Majibu Kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge Kwa Baadhi ya Viongozi Ambao Pia ni Viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge Ikiwa ni Pamoja na Kuwavua Madaraka Yao.
No comments:
Post a Comment