Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, October 17, 2014

MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MAGHARIBI AHUDHURIA MAHAFARI YA KIDATO CHA NNE PHILIP MANGULA SEKONDARI,ACHANGIA MILIONI MBILI ZA UJENZI WA UKUMBI NA KUKABIDHI VITABU 30






 WAAGWA WAKIREJEA UKUMBINI






 MBUNGE NA NAIBU WAZIRI UJENZI  GERSON HOSEA MALANGALILA LWENGE AKIKAGUA MAONESHO YA WANAFUNZI KATIKA SAYANSI




 MKUU WA SHULE YA SEKONDARI PHILIP MANGULA GODFREY MWALONGO  AKISOMA RISALA FUPI YA SHULE KWA MGENI RASMI




 HAWA NI WAAGWA WAKISIKILIZA KWA UMAKINI HOTUBA YA MGENI RASMI




 MGENI RASMI AKIKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE PHILIP MANGULA SEKONDARI

 WATUMISHI NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SHULE WAKIWA KTIKA PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASMI















 Na Michael Ngilangwa-Njombe

Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Gerson Hosea Malangalila Lwenge  Amewaagiza madiwani wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanaingiza kwenye bajeti mpango wa kuanza ujenzi wa bwaro  la chakula katika shule ya sekondari Philip Mangula  Ambpo kukosekana kwa bwaro hilo imesababisha wanafunzi kulilia nje chakula.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi mbaye ni Naibu waziri wa Ujenzi Mhandis Gerson Lwenge wakati akiwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafari ya saba ya Kidato cha Nne   katika shule ya sekondari  Philip Mangula kufuatia kukabiliwa na changamoto hiyo ya bwalo la chakula.

Gerson Lwenge  pamoja na kuwataka Madiwani wa halmashauri hiyo kuweka bajeti  na mikakati kwenye vikao vya baraza la madiwani ya kujenga bwalo la chakula katika shule hiyo pia amewataka wananchi  wa kata ya Imalinyi na Kata nyingine za Taarafa ya Imalinyi kushiriki ujenzi huo kwa kuchangia michango ili kukamilisha mapema Ambapo pamoja na Mambo mengine Ameunga mkono kwa kuchangia shilingi milioni mbili za kuanzia ujenzi huo.

Aidha Mbunge huyo Gerson Lwenge  pia ametoa msaada wa Vitabu 30 vya masomo  mbalimbali vikiwemo vya sayansi  Ambapo amesema changamoto ya kukosekana kwa walimu wa masomo ya sayansi ifikapo mwaka 2015 tatizo hilo litakuwa limekwisha kwani anakwenda kulifikisha wizarani ili kuongeza jitihada za kupeleka walimu wa masomo hayo kwa shule zote za sekondari.

Akitoa taarifa fupi mbele ya Mgeni rasmi  Mkuu wa shule ya sekondari Philip Mangula bwana Godfrey Mwalongo amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi,upungufu wa mabweni mawili,matundu 21 ya vyoo na nyumba 15 za walimu  Jambo linalosababisha   walimu kuishi nje na mahala pa kazi.

Katika risala fupi ya waagwa iliyosomwa na bi.Alumbwage Nyagawa imesema jumla ya wanafunzi 120 wanatarajia kufanya mitihani ya Kidato cha nne mwaka huu ikiwa walianza wakiwa wanafunzi 200 kutokana na sababu mbalimbali imesababisha kufikia idadi hiyo Ambapo  kwa kipindi chote hicho wamekabiliwa na tatizo la kukosa walimu wa masomo ya sayansi ikiwemo fizikia na Hisabati.

Ziara ya Mbunge Na Naibu waziri wa Ujenzi Gerson Hosea Malangalila Lwenge  hii leo inaendelea kwa vijiji vya kata ya Ilembula kukagua Maendeleo ya Mradi wa Umeme  wa REA Ambao umeanza kutekelezwa katika kata hiyo.

No comments:

Post a Comment