Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, October 2, 2014

BASI LA MAPANDA NA UPENDO EXPRESS WAUMANA KATIKA MTO ICHUNILO MJINI NJOMBE MAPEMA LEO









































Watu Watatu Wamejeruhiwa  Na Vibaya  Na Kufikishwa Katika Hospitali Ya Kibena Kwaajili  Ya Matibabu Kufuatia Kutokea Kwa Ajali Ya Gari La Abiria La Kampuni Ya Mapanda Express  Iliokuwa Ikitokea Njombe Kuelekea Jijini Dar Es  Salaam Kuligonga Basi Lililokuwa Mbele Yake Ambalo Ni Mali Ya Kampuni Ya Upendo Na Kusababisha Majeruhi Hao.

Wakizungumza Na Uplands Fm Kwa Nyakati Tofauti  Baadhi Ya Majeruhi Wa Ajali Hiyo 
Wamesema Kuwa Ajali Hiyo Imetokea Leo Majira Ya Saa Kumi Na Mbili  Alfajiri Katika Eneo  La Kona Ya Mto Ichuniro Kuelekea Kibena Wakati Basi La Mapanda Likielekea Jijini Dar   Es  Salaam Na Kusababisha Kutokea Kwa Ajali Hiyo Ambapo Imedaiwa Chanzo Chake Ni  Mwendo Kasi Aliokuwa Nao Dereva Wa Gari La Kampuni Ya Mapanda.

Ajali Hiyo Hiyo Imelikutanisha Basi Lenye Namba Za Usajili T 663 AAH Mali Ya Kampuni Ya  Mapanda Ambalo Limekwenda Kuligonga Basi Namba T 347  APF Mali Ya Kampuni Ya  Upendo  Ambalo Lilikuwa Limepaki Mbele Yake Ndipo Basi La Mapanda Kutokana Na 
Mwendo Kasi Aliokuwa Nao Dereva Wake Likaenda Kuligonga Basi Hilo La Upendo.

Mganga Mkuu Mfawidhi Wa Hospitali Ya Kibena Dr. Patrick Msigwa Amethibitisha Kutokea  Kwa Ajali Hiyo  Ambapo Amesema Miongoni Mwao  Ni    Christina Mbwilo Mkazi Wa Nazareth Na Wengine Wawili Mtoto  Na Baba Mmoja Mkazi Wa Ludewa  Ambaye Amejeruhiwa Kichwani Ambapo  Majeruhi Watatu Ndiyo Waliopokelewa Katika  Hospitali Hiyo Na Tayari Wamekwisha  Ruhusiwa  Kurudi Nyumbani Baada Ya Hali Zao  Kuendelea Vizuri.

Jeshi La Polisi Mjini Njombe Limefanikiwa Kufika Katika Eneo La Tukio Na Kuimarisha 
Usalaama Katika Eneo Hilo Huku Taratibu Za Uchunguzi Juu Ya Ajali Hiyo Zikiendelea.



No comments:

Post a Comment