Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, September 30, 2014

BARAZA LA WAZEE LAIOMBA SERIKALI KUTUNGA SHERIA YA KUCHANA NGUO ZA KUZALILISHA KWA WADADA NA MILEGEZEO KWA WAKIUME HADHARANI

























 MWENYEKITI WA WAZEE KATA YA MAKOGA AKIFUNGUA SHEREHE
 ISKAKA MSIGWA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA PADI




 WAZEE WA KATA YA MAKOGA WAKISIKILIZA KWA UMAKINI
 ABRAHAMU CHAULA NI MGENI RASMI AMBAYE PIA NI DIWANI WA KATA YA MAKOGA

Baraza la Wazee wa Kata ya Makoga  wameiomba Halmashauri  ya  Wilaya  ya Wanging'ombe Mkoani Njombe  kutunga sheria ndogondogo za kuwaruhusu wananchi kuchana Mavazi  ya aibu yanayovaliwa na baadhi ya Vijana wa Kiume na wa kike wakiwemo mabaamedi ili kutunza maadili kwa vijana wengine wasiyo na tabia kama hizo.

Wakizungumza  mara baada ya Maadhimisho ya siku ya wazee kata ya Makoga Wazee hao wamesema kumekuwa na baadhi ya vijana wakiume na wa kike kuwa na tabia ya kuvaa milegezeo ya suruali  na Wasichana kuvaa suruali za kubana na kuchora maumbile yao na sketi fupi zenye mipasuo hususani mabinti wanaouza pombe kwenye grocari yaani mabaamedi  Na kwamba Matendo hayo yanalidharirisha Taifa.

Aidha Wzee hao wameomba serikali za Vijiji,kata na Halmashauri kuwashirikisha kwenye Vikao vya maamuzi,kuwapatia matibabu Bure kama sera ya Taifa Inavyosema kwa vituo vyote vya afya,kuweka mikakati madhubuti ya kudhibiti unyanyasaji wa Kijinsia na Mauaji ya Vikongwe yanayotokana na Imani za Kishirikina pamoja na kuwapatia pesheni za Uzeeni.

Akisoma Taarifa Fupi mbele ya Mgeni Rasmi Muwakilishi wa Baraza la Wazee  Wilaya ya Njombe na Kata ya Makoga bwana Daud Mgeyekwa  Amesema kuwa baraza la Wazee kata ya Makoga lilianzishwa mwaka 2011 chini ya shirika la PADI  Kwa lengo la Kutetea haki za wazee Ambapo limefanikiwa kupata mikopo midogomidogo kupitia shirika la PADI ambayo imesaidia kuendesha miradi ya ufugaji kuku,nguruwe na bustani.


Abrahamu Chaula ni diwani wa Kata ya Mkoga Wilayani Wanging'ombe Akiwa Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho hayo amesema kuwa kuanzia sasa wazee watakuwa wanashiriki kwenye maamuzi ya maendeleo ya kata na kuwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha wanawashirikisha katika kujadili vikao vya ndani pasipo kuwatenga.

Aidha bwana Chaula amesema kuwa kutokana na changamoto zinazowakabili  baadhi ya Wazee  za kutopatiwa matibabu Bure kwenye zahanati zilizoko kwenye vijiji vya kata hiyo wanatakiwa kutoa taarifa kwa uongozi wa kata ili  kumuwajibisha anayeshindwa kuwasaidia wazee kutibiwa bure na kumpeleka kwa Mkurugenzi wake apatiwe adhabu.


Awali akizungumza Mkurugenzi wa shirika la PADI  Iskaka Msigwa  amesema  serikali inalo jukumu la kuwatimizia mahitaji wazee pamoja na Jamii kuwajali kwa kutowanyanyapa,kuwanyanyasa na  kwamba lengo la kuanzisha shirika hilo ni kuwasaidia wazee kupata huduma mbalimbali ambazo zimekuwa haziwafikii wazee ikiwemo matibabu bure.

Maadhimisho hayo ya  Wazee yamefanyikia kijiji cha Uhekule  kata ya  Makoga  Wilayani Wangingombe  huku Mbunge  wa jimbo la Njombe amagharibi akichangia shilingi laki tatu  na mdau wa wazee akichangia shilingi laki moja  ambazo zimekabidhiwa kwa wazee  na diwani huyo Ambapo  leo maadhimisho hayo  kimkoa yanataraji kufanyika katika Taarafa ya Igominyi Mkoani Njombe.

No comments:

Post a Comment