Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, October 12, 2014

ASKOFU ANGLIKANA ATAMANI MRITHI WA RAIS KIKWETE IKULU 2015 ATOKE ZANZIBAR


askofu  mpya wa Dayosisi ya Tanganyika kusini Magharib Methew Mhagama
Mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe akitoa  salam zake
 Waziri  Nyalandu  katika akiwa na askofu mkuu wa Anglikana  Tanzania Jacob Chimeledya  kushoto na askofu  mpya  wa dayosisi ya Tanganyika kusini Magharibi Methew Mhagama na mkewe  leo  baada ya askofu huyo kusimikwa  rasmi
Waziri  wa malisiali na utalii Lazaro  Nyalandu  (mwenye suti wa tano kushoto ) akiwa katika picha ya pamoja na maaskofu wa kanisa la Anglikana Tanzania  na mbunge wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe mwenye suti wa  tatu kushoto ,askofu mkuu wa Anglikana  Tanzania  Jacob Chimeledya ,askofu  mpya wa Dayosisi ya Tanganyika kusini Magharib Methew Mhagama  na  wa  kwanza kulia mkuu  wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba 



WAKATI  hadi   hivi  sasa  makundi  ya  wagombea Urais  yakiendelea  kukitesa  chama  cha mapinduzi (CCM)  kutokana na idadi ndefu  ya  wanachama   wanaotaka  nafasi  ya  kuingia Ikulu  baada ya  Rais Jakaya  Kikwete ,askofu  wa kanisa la  Anglikana Dayosisi ya Tanganyika  kusini Magharibi  Mathew  Wilfred Mhagama ameibuka  na kusema  kuwa  ili  kuliunganisha Taifa la Tanzania  kuwa  moja  ni vema Rais ajaye mwaka 2015 atoke  Zanzibar na si vinginevyo.

" Ninawaomba   sana  wakristo  wa dayosisi  hii na  kote  Tanzania Rais  ajaye  ataongozwa na katiba na  sio  dini  yake   hivyo nawaomba  sana tuheshimu mapatano  yetu  .....   tuombe   vyama  vya siasa  visome  alama  za nyakati  kwa  kutumia vema  maamuzi  ambayo  yataliunganisha Taifa   hili"

Askofu   huyo  alitoa  kauli  hiyo  leo   mjini Njombe  mara  baada ya  kusimikwa  kuwa askofu mpya  wa nane wa  Dayosisi  hiyo baada ya  askofu  aliyekuwepo  kufariki  duni ,sherehe  iliyohudhuriwa na  waziri  mkuu Mizengo  Pinda kwa kuwakilishwa na  waziri  wa maliasili na utalii Bw  Lazaro Nyalandu.

Alisema  kuwa  wito  wake  kwa viongozi  wa umma  wanapokubali kupongezwa  pia  wawe tayari kukosolewa  badala ya  kutangulia kiburi pale wanapokosolewa  hivyo  alisema ni  heri kanisa  kutimiza wajibu  wake kama mtume wa Mungu  kuliko kunyamaza  kimya .

Askofu  Mhagama  alisema  kuwa  Taifa  letu  limekuwa  likipita  katika  mabadiliko   hivyo lazima   waumini wa madhehebu yote  kuendelea  kumwomba  Mungu   ili kufanikisha   kuvuka  salama katika mabadiliko  makubwa  ambayo  nchi  inakwenda  nayo kwa  sasa .

" Ni Lazima  kumwomba  sana Mungu  ili  atusaidie  kutuvusha salama  ilazima  tuombe  bila  kukoma  pia  nashukuru  tume ya Jaji Wariomba kwa  kazi yake nzuri  ya kukusanya maoni  ya  watanzania  katika  mchakato  wa katiba  mpya  uliomalizika  hivi karibuni mjini  Dodoma...... Zanzibar  inahitaji kuzaliwa kwa mara ya  pili  ili  kuepuka na  siasa na  watu kusahau  yaliyopita  kwa  kuwa na  zanzibar  mpya  ya  watu  yenye kuaminiana  na  kuvumiliana  kwani Tanzania  bila  Zanzibar haipo .....uchaguzi  uliopita  nilipiga  kura katika  jimbo langu la Mkunazini  Zanzibar  na kura ya Urais  nilimpigia Dr  Ally Mohamed Shein   wa CCM na  kura ya uwakilishi  nilimpigia Juma  Jusa ( CUF) japo  kuna  wakati  alinikwaza sana  kutokana na kauli zake  ...sikupigia  chama  nilipigia umoja   na  watu  timamu hivyo hekima  za Suleiman  zinahitajika  ili  kulifanya Taifa hili  kuwa mmoja  hivyo Rais  wetu tutakae mchagua  atafungwa na katiba ya  Jamhuri ya muungano wa Tanzania na  sio dini yake  dini itamsaidia  yeye  kuwa karibu na Mungu wake ila katiba  itatusaidia  sisi ambao si wa  dini  yake hivyo ni  vizuri  tukaipa nafasi hekima  ili Rais wa 2015  wa Tanzania atoke  Zanzibar ili isifikie  mahali  Zanzibar  wakaona  wanatumika "

Askofu  huyo  ambae  wazazi wake ni  wazaziliwa wa mkoa wa Njombe  ambao  walihamia  Zanzibar  kikazi ambako pia alizaliwa huko na  kuendelea  kuifanya kazi ya huduma za kiroho huku kabla ya kuchaguliwa  kuwa askofu wakanisa  hilo alisema  kuwa moja kati ya mkakati  wake akiwa katika Dayosisi hiyo ni kuona anaanzisha  mfuko wa kusaidia  watoto  wenye matatizo kielimu na kuwa mfuko   huo  unahitaji kiasi cha Tsh milioni 50 ili  kuanza na  kuwa kamwe hatakubali  kuona  watu ama  mtu anajinufaisha na mali  za dayosisi hiyo ama  vinginevyo kwa faida  yake.

Kwa  upande  wake  mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo  Filikunjombe  akitoa  salam  zake kwa niaba ya  wabunge wa  mkoa wa Njombe  aliwaomba  waumini wa dini  hiyo na madhehebu mengine yote  kuendelea  kuliombea  Taifa  ili  lidumu katika  amani  ,upendo na mshikamano  .

Filikunjombe  alisema  kuwa jukumu la  kuendelea   kuliombea Taifa   hili ni  jukumu la  kila mtanzania  hivyo alisema  kuwa kama  ilivyokuwa katika uchaguzi  wa askofu  huyo  ulifanywa na waumini wake ila  bado maombi ya  waumini wa  dini  zote  yalitawala katika kanisa  hilo  na ndio maana  uchaguzi huo  ulifanyika kwa amani na upendo zaidi .

Pia  mbunge   huyo alipongeza kazi nzuri  zinazofanywa na kanisa   hilo katika  kuwaletea maendeleo wananchi wa Dodosisi hiyo  wakiwemo  wananchi wa  jimbo lake la Ludewa hasa katika  kijiji  cha Mbongo ambako  kanisa hilo  limejitolea  kujenga  Zahanati  na kuwa  huduma   hiyo inasaidia  watu  wote  bila kuangalia  dini  wala  vyama  vyao.

" Niseme  machache  kwa niaba ya  wananchi  wa  Ludewa  wanakuombea kwa mwenyezi Mungu vitu  vitatu ,kwanza kuwa na afya njema na uzima , pili uwe na uvumilivu na zawadi ya tatu  kuendelea  kuwa na busara  zaidi....mwisho niseme mimi ni kiongozi wa mhilimi mwingine  kuna  serikali ,mahakama na bunge naomba sana maaskofu na viongo\zi wote wa  dini  mtuombee  ili mwenyezi Mungu aguse  mioyo yetu na  tuweze kutenda yale ambayo yana saidia  kuwakomboa watanzania  wote"

Akitoa  salam zake kwa niaba ya  waziri mkuu  Pinda ,waziri Nyalandu alisema  kuwa  serikali  ni  sikivu  na  imesikiliza  yote ambayo yanazungumzwa na  wananchi  wake na  kuwa katiba  zote  zitaendelea  kuheshimu  Uhuru wa kuabudu .

Kwani  alisema  kuwa mbali ya  taifa    la Tanzania  kuendelea  kukua kwa kasi ila  zipo  changamoto mbali  mbali ambazo  zimekuwa  zikilikabili  taifa  hasa katika  kundi la  vijana  ambao wameendelea  kudai  kusaidia  changamoto mbali mbali na  kuwa serikali  itafanya kazi ya  kuwaenzi  vijana  hata kama   wamekengeuka  kwa kuwarejesha katika mstari hasa ukizingatia  kuwa vijana ni kiini  cha Taifa  na wakati  huu ni  wakati wa Tanzania  yenye mafanikio kuwadia.

MWISHO

No comments:

Post a Comment